Richard spencer
JF-Expert Member
- Feb 22, 2021
- 1,225
- 1,993
Kujenga tofauti na kuwekeza, Tazara wamejenga sisi ndio tunaendesha shirika tangu kipindi hiko na kuhusu urafiki kiukweli sifaham huko nyuma kilikuwaje ila nafaham walipewa wachina miaka hii na wamefeli. Pia wachina Mao sio sawa na hawa wachina wa leo.Tanzania kampuni gani kubwa ya China Ime invest? Kipindi cha ujamaa kulikuwa na urafiki, Tazara na Project nyengine kubwa hazikuwa zikitoa Ajira na watu kuajiriwa?
Hawa machinga wa China ambao wamejaa siku hizi hawawezi kuwa level moja na Multi Billion corporations.
Unapoongelea projects za Matrilioni ya Hela unatakiwa ufananishe na projects nyengine kama hizo duniani, na sio kufananisha kiduka cha mchina ama viproject uchwara ambavyo kampuni hata haijulikani kimataifa.
Sizungumzii project za matrilioni hapa sababu hakuna aliewekeza hizo pesa hapa Tanzania. Tuchukue mfano kwenye madini, kuna makampuni ya kichina yanachimba hapa lakini huyajui sababu ya ujanja ujanja wao kwenye uendeshaji. Mazingira mabovu kwa mchina sehemu za kazi hayatokani na ukubwa wa uwekezaji bali utamaduni wao, huko kwao kwenye makampuni makubwa wana kitu kinaitwa " 996" ni unafanyakazi hadi unachanganyikiwa.