Afghanistan: Mwandishi wa habari atupwa jela mwaka mmoja kwa kuikosoa Taliban katika mitandao ya kijamii

Afghanistan: Mwandishi wa habari atupwa jela mwaka mmoja kwa kuikosoa Taliban katika mitandao ya kijamii

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Afghanistan-Media-Agencies-880x587.jpg


Mahakama Nchini Afghanistan imemuhukumu mwanandishi wa habari, Khalid Qaderi kifungo cha jela mwaka mmoja kwa makosa ya kuikosoa Serikali ya Taliban katika mitandao ya kijamii, japokuwa Msemaji wa Taliban amesema amehukumiwa kwa makosa ya jinai.

Qaderi ni ripota wa Radio Nowruz amekuwa kizuizini tangu alipokamatwa Machi 2021. Shirikisho la Kimataifa la Waandishi wa Habari (IFJ) limesema mwanahabari huyo chipukizi aliikosoa Serikali kupitia redioni na kwenye mitandao ya kijamii ambapo pia inadaiwa aliiambia Mahakama kuwa alitambua makosa yake na akafuta andiko lake katika ukurasa wake wa Facebook

IFJ imeshutumu hukumu hiyo na kuwataka viongozi wa Taliban kuacha kuminya uhuru wa waandishi tangu walipochukua madaraka Agosti, 2021.

Msemaji wa Taliban, Zabihullah Mujahid amethibitisha kifungo hicho na kusema kuwa hakihusiani na masuala ya uandishi wake.

IFJ imesema: "Chini ya utawala wa Taliban waandishi wa habari wa Afghanistan wameendelea kukabiliwa na vikwazo vikali, vitisho vya uhuru na kukamatwa kiholela." Kundi hilo liliitaka Taliban kumwachilia mara moja mwandishi huyo kutoka gerezani.

Source: VoaNews
 
Ifj ni mashoga tu kama mashoga wengine,
Si heri huyo amefungwa tu tena kijimwaka mmoja tu,
Wa aljazeera juzi ameuwawa kabisa na wao wapo kimya tu
 
Back
Top Bottom