Afghanistan: Rais wa zamani Ashraf Ghani aomba msamaha kwa kukimbia nchi

Afghanistan: Rais wa zamani Ashraf Ghani aomba msamaha kwa kukimbia nchi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Rais wa zamani wa Afghanistan Ashraf Ghani ameomba msamaha kwa watu wa Afghanistan baada ya kukimbilia katika nchi za Falme za Kiarabu.

"Kuondoka Kabul ulikuwa uamuzi mgumu zaidi maishani mwangu," amesema, akiongeza kuwa anajuta kwamba "hakuweza kumaliza hilo kwa njia tofauti."

Bwana Ghani aliondoka ghafla nchini Afghanistan wakati wanamgambo wa Taliban walipokuwa wakiendelea kuingia kwenye mji mkuu mnamo Agosti 15.

Alisema hakuwa na nia ya kuwaacha watu wake lakini "ilikuwa ndio njia pekee iliyosalia."

Katika taarifa iliyoshirikishwa kwenye mtandao wa Twitter siku ya Jumatano, Bw. Ghani alisema hakuwa na njia nyingine yoyote zaidi ya kuondoka nchini humo ili kuepusha kuenea kwa ghasia.

"Niliondoka kwa kushawishiwa na usalama wa ikulu, ulionishauri kuwa kuendelea kuwepo kulihatarisha kutokea kwa mapigano mitaani na katika barabara za mji kama ilivyotokea wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka ya 1990," aliandika, akiongeza kuwa alifanya hivyo "kuokoa mji wa Kabul na raia wake milioni sita".

Alisema alikuwa amejitolea kwa kipindi cha miaka 20 kusaidia Afghanistan kuwa "nchi ya kidemokrasia, mafanikio na huru."

Bwana Ghani ameongeza kuwa alikuwa na "masikitiko makubwa" kwamba "muda wangu mwenyewe uliishia kwa majuto kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wangu."


Chanzo: BBC swahili
 
Kuondoka Kabul ulikuwa uamuzi mgumu zaidi maishani mwangu," amesema, akiongeza kuwa anajuta kwamba "hakuweza kumaliza hilo kwa njia tofauti."
[emoji848][emoji848][emoji848][emoji1541][emoji1541][emoji1541]
Yale mabilioni atayarudisha?
 
Huko watu wanazidi kuikimbia nchi yao, tena wengi sana hata hivi leo wanaendelea kukimbia

Sijajua Taleban wanaogopwa nini?
 
Huko watu wanazidi kuikimbia nchi yao, tena wengi sana hata hivi leo wanaendelea kukimbia

Sijajua Taleban wanaogopwa nini?
Raia hawawaogopi Taliban ila sharia za kiislamu ndio shida. Zinawabana sana ukizingatia mambo yamebadilika sasa hivi ila sharia zao zinawataka waishi kama wahenga wao😄😄 hata mimi ningekuwa mmoja wa wakimbiaji.
 
Taliban are the false preachers, preaching water to their people while taking wine to themselves.
 
Back
Top Bottom