Afikishwa Mahakamani kwa kumbaka na kumuambukiza VVU mtoto

Afikishwa Mahakamani kwa kumbaka na kumuambukiza VVU mtoto

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Deogratias Wiliam (45) Mkazi wa Mombasaraha Kata ya Butundwe Wilaya ya Geita amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu mkazi Geita akishtakiwa kwa makosa mawili ya kumbaka na kumuambukiza Virusi vya Ukimwi mtoto wa miaka 17.

Mbele ya hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Nyakato Bigirwa Wakili wa Serikali, Godfrey Odupoy akishirikiana na Kabula Benjamen ameieleza Mahakama kuwa mshatakiwa huyo anadaiwa kutenda makosa hayo kwa tarehe tofauti kati ya mwaka 2018 hadi 2023.

Wakili Odupoy ameieleza Mahakama kuwa mshatakiwa ametenda kosa la ubakaji kinyume na kifungu 130(1&2e) na 131(1)cha kanuni ya adhabau ambapo huko Mombasaraha katika tarehe na nyakati tofauti Deogratius alifanya mapenzi na mtoto wa miaka (17) ambae jina linahifadhiwa.

Katika shtaka la pili katika kesi hiyo namba 57/2023 mshtakiwa anadaiwa kusambaza virusi vya ukimwi kinyume na kifungu namba 47 cha sheria ya kuzuia virusi hivyo.

Imedaiwa kuwa kwa tarehe tofauti ndani ya mwaka 2018 hadi 2023 mshatakiwa akiwa eneo la Mombasaraha kinyume na sheria na kwa makusudi alimuambukiza mtoto huyo Virusi vya Ukimwi.

Mwendesha mashtaka wa Serikali aliieleza Mahakama kuwa ushahidi wa kesi hiyo umekamilika na kuomba tarehe kwa ajili ya kuja kusoma hoja za awali.

Mshatakiwa alitakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaosaini hati ya Sh5 milioni kila mmoja pamoja na kuwa na barua za utambulisho, hata hivyo alishindwa kukidhi masharti ya dhamana na kupelekwa mahabusu huku, kesi hiyo ikiahirishwa hadi Julai 5, 2023 itakapokuja kwa ajili ya hoja za awali.

MWANANCHI
 
Inabidi Immigration iende Geita ikawafurumushe wahamiaji haramu. Kuna tabia zingine sio za kitanzania kabisa. Makatili waliopo Geita waondolewe
 
Kama macode yanasoma na binti kweli ameambukizwa imethibitika basi wamalizane naye tu jamaa aende akapumzika mbinguni.
 
Back
Top Bottom