Afisa Ardhi auawa Kilombero kisa mgogoro wa Ardhi

Frank Wanjiru

Platinum Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
25,686
Reaction score
46,842
Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linachunguza mauaji ya Afisa Ardhi wa Wilaya ya Kilombero, Zakaria Rashid Malika (57), aliyefariki baada ya kuvamiwa nyumbani kwake na watu wasiojulikana.

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, tukio hilo lilitokea usiku wa Julai 19, 2026 katika Kitongoji cha Kapolo CCM, Kata ya Kibaoni, ambapo marehemu alijeruhiwa kwa kitu chenye ncha kali katika sehemu mbalimbali za mwili hadi kupoteza maisha.

Uchunguzi wa awali unaonyesha chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa muda mrefu wa ardhi kati ya marehemu na wenzake.

Polisi wanawashikilia watu wawili kuhusiana na tukio hilo huku uchunguzi ukiendelea.
 
Uchunguzi wa awali unaonyesha chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa muda mrefu wa ardhi kati ya marehemu na wenzake.
Nilijua tuu
 
Madhara ya ufisadi na kuchukua sheria mkononi
Huyu kauwawa na wenzake wanafungwa jela, wote wanakosa kumiliki hiyo ardhi
 
Mkuu hawa jamaa wanaumizaga sana wananchi m nikishawahi kwenda arusha kulilia kiwanja chang afisa alienisaidia kununuyuleyule akatakakuuza kwa mtu nkaenda kwa makonda..yaan na docs zote na walinipa Kibali kujenga..nkajenga msingi jamaa akanza kupandisha nkashtuliwa aisee nilimwambia yule jamaa Mungu amenisaidia nimerudisha kiwanja chang utaadhibiwa hutoamin

akatupwa kiteto 1
2.mwanae akaumwa kama mlisikia aliepelekwa hospt jamaa wakamfumua kichwa kumbe kaenda na issue ya mguu

Wakamkimbiza India akaishia huko

MUNGU AMLAZE PEMA PEPONI MAREHEMU

NASIKILIZA HAPA ITV MAREHEMU AMEACHA MKE NA WATOTO 10

AFISA ARDHI NAKUPONGEZA KWA HILO JAMAN
 
Aridhi haijawahi kumwacha mtu salama.
Marehemu kaacha watoto 10.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Inashangaza kuona kwenye nchi hii waliosoma wanaongoza kwa kukosa utu. Migogoro mingi ya ardhi mitaani wahusika ni hawa washua wa miaka 40s na 50s. Sijui wana shida gani hawa jamaa.
 
umri huo na nimtumishi kwenye ardhi Hana ardhi isiyo na mgogoro

mnawatukanaga walimu Bure tu
 
Kiufupi ni Tamaa ,hao wenzake ni kina nani ,maafisa wenzie,raia au wenzake kivipi ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…