Afisa Ardhi Kanidhulumu, naweza kumfukuzisha kazi ila nikikumbuka watoto wake na mke wake nashindwa kuchukua hatua

Afisa Ardhi Kanidhulumu, naweza kumfukuzisha kazi ila nikikumbuka watoto wake na mke wake nashindwa kuchukua hatua

mwanyaluke

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2015
Posts
704
Reaction score
2,435
Ipo hivi, Nina mshikaji wangu ni Afisa Ardhi (sitaweza taja halmashauri yake) nimesoma naye chuo degree ya Sheria, mwenzangu alibahatika kuwa afisa ardhi.

Alinipigia simu anataka simu kuwa Wana uwanja unafaa kwa uwekezaji wa kituo cha mafuta, niliwatuma vijana wangu wakauona ule uwanja , then wakaniambia yes tunaweza funga kituo hapo, basi nikambiwa uwanja unauzwa milioni ishirini.

Nikampatia pesa hiyo, baasi nimekaa wiki hii nimepita eneo lile nakuta kuna materia zipo pale, nakuliza wanasema kuna mtu anataka kujenga hotel.

Nimefanya jitihada ya kumpata anayetaka kujenga , amenijiibu lile eneo alinunua na ana hati , na mimi nililipa na Nina hati, nimemtafuta jamaa afisa ardhi anatoa very very lame idea.

Nimemwambia arudishe pesa hana, nikifikiria umri wa mshikaji na aina ya familia inanichanganya but no way pesa yangu irudi.
 
Mi naona mliuziana kishkaji asingekugeuka usingetusimulia, pambaneni hata mkiuana poa tu
 
Back
Top Bottom