Afisa bank ananiambia namharibia kazi kisa kuchelewesha repayment..is this serious??

gidume

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2017
Posts
743
Reaction score
915
Katika mihangaiko yetu ya kujikwamua kiuchumi hatimae nimeingia kwenye mikono ya mikopo ambayo kimsingi hali ya uchumi ilivyo haikwepeki.

Bahati nzuri repayments zinafanyika vyema ila mwezi huu kidogo mambo yamekua tyt kiasi kwamba nimedeposit kiasi kidogo cha fedha nje ya maagano yangu na bank na mda umezidi week nzima kabla sijafanikiwa kumaliza repayment nikiwa nategemea kumalizia ndani ya siku hizi mbili..

Maajabu yametokea hapa..

Kwanza akipiga simu kukumbusha rejesho hamna maelewano mazuri hata ukianza na salamu ya mambo anajibu mabaya [emoji38][emoji38].

Kisa nini kwan hujui hujamalizia rejesho.hee vitaa.

Juzi akaniambia nifate barua..he kuuliza barua ya nini eti ya kuvunja mkataba akanijibu lakini I thought wasn’t serious ni ili niwahishe kufanya repayment.

Baada ya kudeposit kiasi cha asilimia 75 kesho yake kanipigia simu “mbona hujamalizia installment.unajua unaniharibia kazi,kwann unapenda kazi yako alaf kazi za wenzako hupendi.

Wenzetu mliokua katika hii field tusaidiane..ivi ni kweli kwamba kudai installment na kuchelewesha kufanyisha installment kunaweza fukuzisha mtu kazi

Izi treatment katika kudai ndo mnaambiwa mfanye hivi au tabia tu ya mtu..tuwekeni wazi kwa sbb kipindi cha kuomba mtukope mnatubembeleza sana [emoji23][emoji23]

Nawasilisha..
 
dawa ya Deni Ni kulipa.... ila pole mkuu
 
Mkuu hakuna kitu kama hicho,Mimi huwa namblock kimbelembele kama huyo huku nikiendelea na kulipa taratibu na siku nyingine anakuwa na adabu ila changamoto ukitaka kukopa tena lazima atakuletea kimavi!cha msingi ni kutojibu SMS zake wala call zake
 
Badala umshauri mwenzio aogope kuchelewesha kulipa we unamshauri amblock mdai jamani.

Hawa watu Wana Target za kukusanya madeni, kweli wasipofika target kazi zao zinakuwa hatarini Sana.

Sikushauri kabisa mdaiwa kuacha kupokea simu au kumblock. Utafanya watafute njia mbadala ya kudai fedha zao ambayo lazima itakuwa mbaya kwako!
Mkuu hakuna kitu kama hicho,Mimi huwa namblock kimbelembele kama huyo huku nikiendelea na kulipa taratibu na siku nyingine anakuwa na adabu ila changamoto ukitaka kukopa tena lazima atakuletea kimavi!cha msingi ni kutojibu SMS zake wala call zake
 
Naomba kuuliza hv kwa mfano ukishindwa rejesho labda kwa miezi 2 h wanaweza piga bei dhamana yako? au baada ya muda wa mkopo kuisha ukishindwa kulipa pesa yao ndio wanapiga bei?
 
Mkuu hakuna kitu kama hicho,Mimi huwa namblock kimbelembele kama huyo huku nikiendelea na kulipa taratibu na siku nyingine anakuwa na adabu ila changamoto ukitaka kukopa tena lazima atakuletea kimavi!cha msingi ni kutojibu SMS zake wala call zake
Mkuu Muuza Simu used naweza kusema mshauri vizuri mtoa mada. Kwa ninachojua kuchelewesha rejesho ni moja ya sababu yakutokopeshwa tena au kupunguziwa mkopo pindi akitaka kukopa tena hasa kama ucheleweshaji umekuwa ni wa mara kwa mara. Kuhusu kuhatarisha kazi ya afisa wake hiyo ni kweli kwani afisa mikopo anapimwa kwa mikopo anayotoa na mikopo aliyotoa inalipikaje (Mikopo chechefu kwa kikinga wanaita PAR yaani portifolio At Risk na NPL yaani Non perfoming Loans).
Sasa basi hapo lawama bado znarudi kwa mteja ambaye ni mtoa mada kwanza kwa kuchelewesha rejesho pili kwa kushindwa kutoa taarifa ya kuchelewesha rejesho. Kama kweli mtu upo serious na biashara na unampango wa kukua kibiashara sidhani kama utamblock afisa mikopo wako na kumuona kihelehele wakati anafanyakazi yake na alikukopesha kiroho safi.
Hivi nani saiz anaweza kukuazima milioni tano? Lakini ukiwa na sifa za kukopesheka unaenda benk unavuta mpunga. Hivyo basi tujijengee sifa nzuri za ulipaji mzuri kwenye mabenk na sacos na kwingine tunakokopa kwani ndio njia rahisi ya kukuza mitaji yetu. Jioni njema
 
Naomba kuuliza hv kwa mfano ukishindwa rejesho labda kwa miezi 2 h wanaweza piga bei dhamana yako? au baada ya muda wa mkopo kuisha ukishindwa kulipa pesa yao ndio wanapiga bei?
Mkuu inategemeana na benki au taasisi yako. Pia soma mkataba wako unasemaje shida tukiwa nashida na hela ile mikaratasi hatusomi tunatafuta sehemu ya kusaini na kuandika tarehe basi. Kuna benki wao ni siku 90+ wanauza dhamana ila hadi ishu inafika kwenye kuuza dhamana mara nyingi mteja anakuwa amesumbua kwani mnaweza kuangalia namna ya kumaliza deni bila kuathiri dhamana sasa kama wewe ndio unaona maafisa mikopo wako vihele hele lazma dhamana ipigwe mnada tu
 
Hpo umeongea tukiwa na shida hatusomi mikataba vizuri!
 
Mkuu hakuna kitu kama hicho,Mimi huwa namblock kimbelembele kama huyo huku nikiendelea na kulipa taratibu na siku nyingine anakuwa na adabu ila changamoto ukitaka kukopa tena lazima atakuletea kimavi!cha msingi ni kutojibu SMS zake wala call zake

Powa powa kaka
 


Hebu acha kucheka cheka hovyo na kuweka vi-emoji wakati unadaiwa...hebu lipa tafadhali.

On a serious note...achana na tone ya huyo jamaa...jikite kwenye kulipa tu na jitahidi kum-manage maana watu tuna tofautiana sana.

Pia, hongera kwa kukopa na kufanya mishe...watu wengi wanaogopa madeni

All the best
 

Kabisa kaka asante kwa ushauri..lakin waboreshe treatment zao duh..wanatutisha wateja..nna miaka mitatu ktk hili suala lkn naona mungu akibariki nijamaliza bora nipumzike kidogo..nshasense hatari.
 
mkuu gidume ni kweli unaweka kibarua cha afisa katika hali ngumu,kwa sababu anakuwa anagongeswa na meneja na PAR yake ina shoot, Bank nyingi wanaangalia perfomance ya afisa kutokana na Portfolio yake. fikiria ikiwa wateja kamaa wewe wako sita wamelipa hizo asilimia,je portfolio at risk ya huyu afisa itakuwa kubwa kiasi gani?mkopo uko hivi mfano unaweza kuwa umekopa milioni kumi, kwa mwaka na rejesho lako labda ni laki 600000 kwa mwezi,ukilipa 599900,bado inaonekana unadaiwa rejesho lote. kumbuka ni system sio manual
 

Asante mkuu [emoji120][emoji120]
 

Okay sawa sawa..nashkuru nimefanikiwa kumaliza..sbr nipambane ya mwezi ujao nisimuangushe..
 
Ni kweli...wengine hawakulipi Hadi mteja alipe. Wengine wanalipwa kwa commission... wengine wanawekewa target
 
Mkuu hapo huna jinsi ni kulipa tu kulingana na mkataba hayo mengine wala hata hayatakusaidia!! Kwani loan officer, ni jukumu lake kukusimamia na kuhakikisha kuwa una rejesha marejesho kama mkataba unavyosema!! Huwa hakuna sababu nyingine tena inayokubalika kwa kushindwa kwako kurejesha hata uweumerejesha 99% hiyo asilimia moja tu inaweza ikakugharimu!!
 
Shukrani kwa jibu lako mkuu,lakini nimeongea kwa experience yangu mwenyewe na mikopo,kwa kifupi sidhani kama kuna mfanyabiashara anayependa achelewe kulipa marejesho ila hili sometimes linatokea kwenye biashara, sasa tatizo unakuta anayekusimamia ana kiherehere kama Mke wa balozi anakupigia Simu kama TALA na ikumbukwe kuwa unapochelewa kulipa unalipia na faini sasa unamuelewesha anayekusimamia mkopo ABC lakini anakuwa hataki kukuelewa anaendelea tu kukupa stress,nilichofanya nikampa ban moja matata na mkopo nikamaliza fresh,sasa nilipokuwa nataka kukopa tena akaanza kumjaza maneno meneja wa Bank ili nisipewe mkopo,lkn meneja kuangalia kwenye system wakakuta ni ucheleweshwaji wa kawaida tu,na akaambiwa chuki binafsi usilete kwenye kazi Mzee nikavuta tena mpunga na nikabadilishiwa msimamizi hadi Leo heshima, mdoa mada namshauri ampe tu ban moja matata na aendelee kurejesha marejesho yake kama kawaida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…