Afisa elimu mkoa wa Geita afariki ghafla kikaoni

Afisa elimu mkoa wa Geita afariki ghafla kikaoni

Superbug

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
13,864
Reaction score
35,079
Afisa elimu mkoa wa geita Julius Nestory amefariki ghafla kikaoni. Taarifa zitawajia punde.

===
Ofisa Elimu Mkoa wa Geita, Julias Nestory amefariki ghafla wakati akiwa kwenye kikao na maofisa elimu wa wilaya kilichofanyika katika Shule ya Sekondari Nyankumbu iliyopo mjini Geita.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Geita, Glory Urio amethibitisha kifo hicho na kusema alifikishwa hospitalini hapo majira ya mchana akiwa kwenye hatua za mwisho za uhai.

“Ni kweli tumempokea akiwa kwenye hatua za mwisho tumejitahidi kuokoa maisha yake lakini imeshindikana,” amesema Urio

Katika taarifa ya ofisa habari mkoa, Paul Zahoro inaeleza kuwa ofisa elimu huyo ameugua ghafla wakati akizungumza na maofisa elimu na kukimbizwa katika hospitali ya mkoa kwa matibabu na kufariki akipatiwa huduma ya kwanza
 
Kuna nyuzi kadhaa humu,
Marehemu amewahi kulalamikiwa Sana na watumishi wake humu ndani.

Huenda walamikaji wameamua tu kumpandisha cheo akawe kiongozi MWENDAZAKE kule majuu.

R .I.p
Madaraka yanatutoa ufahamu
 
Back
Top Bottom