A
Anonymous
Guest
Kumekuwepo na malalamiko ya muda mrefu katika Halmashauri ya Momba kutoka kwa Walimu na wadau mbalimbali juu ya tabia na mwenendo kutoka kwa kiongozi huyu.
1. Walimu wengi wamehamishwa bila kufuata utaratibu na malipo ya uhamisho imekuwa ni shida sana kulipwa.
2. Ari ya walimu kufanya kazi imeshuka kutokana na vitisho kutoka kwake.
Anapotembelea shule zake anaacha sintofahamu kwa walimu na hasa walimu wakuu kwakuwa lugha anazotumia si rafiki kabisa kwani ni lugha mbaya na kutishia kuwatengua walimu wakuu hao kila mara na baadhi ya walimu wakuu wameamua kuachia nafasi zao kutokana na vitisho na kero toka kwake.
3. Ametengua walimu wakuu wengi kwa kisingizio cha kwamba hawawezi kazi lakini bado hakuna kilichobadilika. Mfano kuna walimu waliotenguliwa karibu kabisa na mitihani ya Taifa na bado akawataka wapokee ugeni wa mitihani na kuna wengine amewatengua kwa kisingizio cha kutosimamia miradi ya ujenzi lakini bado pamoja na kuwatengua amewataka waendelee kusimamia miradi hiyo.
4. Wapo walimu wakuu waliopitia shida hizo za usimamizi wa miradi kutokana na amri zake za hovyo tena bila kutumia maandishi yoyote katika maagizo yake. Kuna walimu wakuu wametumia pesa zao kukamilisha miradi kwasababu ya kupotezwa na Kiongozi huyo kutokana na vitisho vyake kwamba yeye ndiye boss hivyo hawatakiwi kupinga. Kuna walimu wakuu walikuwa na miradi ya thamani ya Mil.50 tu lakini wakalazimishwa kununua saruji kiwandani ambapo gharama za usafiri zikaja kuwa kubwa sana na kupelekea hasara.
5. Lakini amefikia hatua hata Idara zingine hazitambui katika usimamizi wa miradi kwa kuwaamrisha walimu wakuu kutekeleza maagizo yake bila utaratibu.
6. Walimu wanakerwa na tabia yake ya kujiona Mungu mtu na kusimulia maisha yake kila mara wanapoitwa kwenye vikao vyake na pia ziara zake zimekuwa ni za vitisho na hii imepelekea walimu wengi kuvunjika moyo wa kufanya kazi na hata matokeo ya mtihani wa Taifa darasa la Saba kushuka inaweza kuwa ni moja ya sababu.
7. Kwa kawaida kiongozi anapotaka aogopwe kwa vitisho anavyotoa kwa walimu na walimu wakuu maana yake kuna jambo limejificha nyuma yake. Mfano; kama amepewa pesa za kuhamisha walimu 10 anahamishaje walimu 20? Na kwanini walimu wanalipwa pesa za uhamisho kwa mafungu? Na kwanini walimu hawalipwi pesa zao stahiki na badala yake wanalipwa pesa za nyanya?
8. Kuna michango ya shule kuchangia michezo ya UMITASHUMTA, shule zikichangia bado anarudi kutoa vitisho na kuwataka walimu wakuu wachangie tena pesa na mazao nje na utaratibu kwa kisingizio kuwa pesa hazitoshi japo hakuna siku tathmini imefanyika kubaini matumizi ya pesa hizo.
Tunaomba mamlaka zimchunguze huyu Kiongozi kwasababu hata alikotokea (Songwe DC) amewaachia watu makovu kutokana na tabia zake. Atambue kuwa uongozi siyo vitisho na anaowaongoza ni watu wazima wenye familia na wanategemewa na familia zao. Waliomteua walitumia kigezo gani? Au ndiyo kujuana?
Kiongozi huyu hafai hata kuwa Mwalimu mkuu wa Shule yoyote ile kwasababu hana utu kabisa na ni katili asiye na maana yoyote. Amekuwa mtu anayejijali yeye tu na kuwafokea watu wazima wakiwemo Maafisa Elimu Kata ila tu wanaogopa kumwambia kwasababu wanalinda vyeo vyao. Mamlaka msipuuze jambo hili na mkitaka fikeni Momba DC mfanye uchunguzi.