Mtaka Chake
New Member
- Sep 20, 2026
- 2
- 3
Hivi karibuni kumekuwepo na vitendo vya ukiukwaji wa sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma unaofanywa na Afisa Elimu Sekondari wa Wilaya ya Serengeti.
Ukiukwaji wa sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma unaondoa haki za watumishi na kusababisha uonevu pamoja na manyanyaso.
1. Kuhusu uhamisho wa walimu wa Ikorongo Sekondari
Ijumaa, tarehe 18/09/2026, Afisa Elimu huyo alitoa barua za kuwajulisha walimu watano (5) wa Ikorongo Sekondari kuwa wajihamishe.
Afisa Elimu huyo alienda shuleni na kuitisha kikao na wanafunzi, ambapo aliwaomba wataje walimu wanaodaiwa kuwa na mahusiano na wanafunzi. Baada ya baadhi ya walimu kutajwa, aliwaambia kuwa hataki maelezo yoyote na kwamba wanapaswa kuhama kwenda vituo atakavyowapangia.
Hadi sasa, walimu hao wanahaha bila kuwa na fedha za kutosha za kuhama, huku wakitakiwa kwenda katika vituo vilivyo mbali takribani kilometa 50. Baadhi yao wana watoto, mizigo na mifugo ambayo pia inahitaji kusafirishwa. Hali hii imekuwa chanzo cha mateso na manyanyaso kwa walimu hao.
2. Kuhusu tukio la mwalimu wa Robanda Sekondari
Mkuu wa Shule ya Robanda Sekondari alimpigia simu Afisa Elimu huyo na kumjulisha kuwa kuna mwanafunzi aliyefika shuleni kuchukua cheti chake. Mwanafunzi huyo alikuwa amemaliza Kidato cha Nne mwaka 2024.
Baada ya kuchukua cheti, mwanafunzi huyo aliondoka na baadaye akaolewa na mwalimu. Afisa Elimu huyo alimpigia simu mwalimu huyo na kumtaka afike katika ofisi yake. Baada ya mwalimu kufika, alipelekwa kituo cha polisi na kuwekwa selo kwa tuhuma za ubakaji.
3. Tuhuma za kuomba mahusiano na walimu wa kike
Pia, Afisa Elimu huyo huwaomba walimu wa kike kuwa na mahusiano naye kwa ahadi ya kuwapa vyeo. Mwalimu anayekataa ombi hilo, hasa akiwa Mkuu wa Shule, huandaliwa mazingira ya kuondolewa kwenye nafasi yake.
Mfano unaotajwa ni wa aliyekuwa Headmistress wa Chief Salota Sekondari, ambaye alitengenezewa zengwe kwa tuhuma kwamba alitumia vibaya fedha au vifaa vilivyohusiana na mifuko 200 ya saruji iliyokuwa imeletwa kwa ajili ya ujenzi wa mabweni, licha ya kwamba mabweni hayo yalikuwa yamekamilika.
Ombi kwa mamlaka husika
Naomba mamlaka husika zichunguze kwa kina tuhuma hizi pamoja na namna Afisa Elimu huyo anavyotekeleza majukumu yake. Uonevu na manyanyaso dhidi ya walimu kuwa makubwa kuliko kawaida.
Walimu wanapolalamika kwa Mkurugenzi, wanaeleza kuwa hawapati msaada wa kutosha, hali inayowafanya waendelee kuhaha na kuteseka katika mazingira ya kazi.
Naomba suala hili lifanyiwe uchunguzi wa haki na wa kina ili kubaini ukweli, kulinda haki za watumishi na kuhakikisha sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma zinafuatwa.