Afisa Elimu, Wilaya ya Mbinga, alistahili kufukuzwa kazi na sio kupewa Demotion

Afisa Elimu, Wilaya ya Mbinga, alistahili kufukuzwa kazi na sio kupewa Demotion

ligera

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2014
Posts
2,646
Reaction score
1,171
Katika ziara yangu niliyoifanya mwaka jana wilayani mbinga niliandika thread juu ya madudu aliyoyafanya afisa elimu msingi wilaya ya Mbinga bwana David Mathias Mkali kuiba fedha za halmashauri yeye na msaidizi wake afisa elimu vifaa na takwimu bwana Kapinga.

Ile thread niliyoiandika hapa jf kwamba afisa huyo na swaiba wake bwana Kapinga walikuwa wanashirikiana kuchangisha fedha kwa wazazi na kuzitumia kwa matumizi yao binafsi walistahili kufukuzwa kazi wote wawili.

Lakini cha ajabu afisa elimu huyo wa msingi amepewa demotion na ameenda kuripoti shule ya msingi Burundi kata ya Matiri wilaya ya Mbinga kama mwalimu wa kawaida. Hiyo adhabu haitoshi kwani ameiba fedha nyingi na alistahili kufukuzwa yeye na mwizi mwenzake Kapinga wa ofisi ya vifaa na takwimu.

Inakuwaje afisa mwizi aliyekuwa anaingiza fedha kwenye akaunti za shule halafu jioni anawapigia simu walimu wakuu kuzitoa fedha hizo zote na kumpelekea bar yeye na swaiba wake Kapinga, amefanya hivyo kwa shule nyingi tu.

Anawasainisha waratibu posho ya kikao laki saba halafu anawapa bahasha yenye shilingi elfu 35 anawaambia wakafungulie mbele ya safari, atakayelalamika anamvua madaraka, waratibu wengi wamevuliwa madaraka kwa vitendo vyao vya kudai haki zao.

Adhabu aliyopewa huyo afisa elimu msingi ni ndogo na hakuna sababu yoyote ya kumwacha Kapinga pale ofisi ya vifaa na takwimu wakati kuna ushahidi wa wazi kwamba wote ni wezi.

Tunaishukuru JamiiForums, pamekuwa mahali ambapo madudu mengi ya viongozi yanaanikwa hapa na wanaotuhumiwa wanafanyiwa uchunguzi na hatua zinachukuliwa dhidi yao. Kashfa ya escrow zilianzia hapa , kashfa za ajira za Uhamiaji na scandal nyingi tu.
 
Mwalimu wangu Mathias Mkali mseto s/m, ulikutwa na nini? hukuridhika na marupurupu yote? Pole unarudi kushika chaki cheo umekitumikia kwa mda mfupi sana aiseee.
 
Wanipe mimi basi hyo chance niwaadabishe...na nikipangiwa hyo shule hakika atajuta kunifahamu huyo mchakachuaji wa fedha za umma pamoja na PAYE yangu
 
Kushushwa cheo/mshahara ni adhabu ya juu katika utumishi wa umma na vipo vigezo kadhaa kufikia uamuzi huo. Kufukuzwa labda kosa kwa kosa la jinai.

Labda km vigezo havikufuatwa hapo sawa, tatizo huwa nani amvike paka kengele(kutoa ushahidi bila shaka).
 
Mwalimu wangu Mathias Mkali mseto s/m, ulikutwa na nini? hukuridhika na marupurupu yote? Pole unarudi kushika chaki cheo umekitumikia kwa mda mfupi sana aiseee.

Alikutwa na nini mkuu.
 
Wanipe mimi basi hyo chance niwaadabishe...na nikipangiwa hyo shule hakika atajuta kunifahamu huyo mchakachuaji wa fedha za umma pamoja na PAYE yangu

Mkuu inaonekana ukipelekwa shule hiyo ukawe mwl mkuu hutampa hata utaaluma .
 
ligera,

kutoka kuwa mkuu wa idara hadi mwl wa kawaida ni sawa na kufukuzwa. wameona wakimfukuza anaweza peleka kesi mahakamani ambapo akishinda inakuwa faida kwake kulipwa fidia.

lzm ataacha kazi au atashindwa kufundiaha ndo atafukuzwa.
 
Last edited by a moderator:
Hizo ni tuhuma tu na ndio maana hata mleta uzi ameishia kutaja bahasha zenye elfu 35 tu. DEO Msingi alikuwa makini kwenye ulaji na ndiyo maana kumfukuza imekuwa ngumu wameishia kumpeleka sehemu ambayo anajishikiza wakati miradi yake kwa kila siku inaingiza mshahara wa mkuu wake wa shule mnadhani atamfanya nini hata kama asipoingia darasani?

Big up mkali umekula urefu wa kamba yako, wao wakila Escrow wewe kamua ulipo nyumba ikianguka itafunika wote.
 
Mwalimu wangu Mathias Mkali mseto s/m, ulikutwa na nini? hukuridhika na marupurupu yote? Pole unarudi kushika chaki cheo umekitumikia kwa mda mfupi sana aiseee.

Mkuu; maadili ni janga la Taifa zima. Tumesahau ukweli wakwamba, "Taifa ni watu, ......". Sasa mtu anakuwa mbaya kias hicho bila sababu ya msingi. Urafi tu.

Utakuta wakati akiwa mwalimu wa kawaida zamani ndiye huyohuyo aliykuwa akiongoza #migomo ya CWT kudai hakhi. Leo hii nfyuuuuuuu!!

Halafu mtu anakuja anasema CCM imechoka!

It begines with you. Start now. Hakuna malaika atakayekuja kutulindia rasilimali na maadili. We have to be serious right from our minds.
 
ligera,

Mkuu alianza kushughulikiwa kapinga yeye ni mwalimu wa sec ya ukata kata ya ukata.
 
Last edited by a moderator:
ligera,

Mbona hiyo adhabu ni kubwa sana! Ulitaka auawe au kakuchukulia dem!?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu,

Naona umeandika kwa jazba sana kuhusu suala la bwana Mkali. Ni kweli lazima tukiri wazi kuwa kuna mambo mbwana mkali hajafanya vizuri lakini kuna mambo amejitahidi sana. Lakini suala lake kuna giza nene ambalo mimi na wewe hatulijui ila kuna jambo zito lipo nyuma ya pazia.

Labda nikukumbushe tu kuwa Mkali alihamia Mbinga akitokea Tunduru ambako alisaidia sana kuipushi kielimu wilaya ya Tunduru hadi kufikia kushika nafasi ya 2 kimkoa...je unalijua hilo. Wakati huo wilaya ya mbinga kwa mitihan darasa la saba ilikuwa ikishika nafasi ya mwisho kimkoa tena mara 2 hadi RAS alikuja juu na kuwaandikia barua ya onyo kali...unalijua hilo?

Ujio wa mkali mbinga umesaidia sana kuinua wanambinga kielimu..hasa elimu ya msingi. Mimi nilikuwa Mbinga nafanya utafiti....katika shule za msingi na wadau wangu walikuwa walimu washule za msingi....it was so amazing! walimu wapo committed na kazi, well organized and very cooperative.....tofauti na wilaya nyinginezo kama 11 hivi nilizopitia.

Kielimu...na hasa ukichukulia matokeo haya ya std seven for 2 years mbinga wapo juu kuliko wilaya zote za mkoa wa Ruvuma. Na wilaya ya mbinga ina shule zaidi ya 220 ukilinganisha na wilaya nyinginezo ambazo hakuna wilaya yenye shule hata 130 kwa mkoa wa Ruvuma.

Hivi...mtoa mada unazani ni rahisi kwa shule ya msingi KITAI iliyopo pale porini..kati ya mbinga na songea kushika nafasi ya kwanza kimkoa.....do you think it is easier?? kwanini isiwe songea manispaaa wenye shule za mjini na walimu wa kumwaga??


NB: Nikusaidie tu.....Mkali alikuwa na bifu zito na mkurugenzi wake bwana Ngaga, hivyo sio rahisi mafahari wawili waishi kwenye zizi moja.

Jaribu kujiongeza mkuuu !
 
Big up deo kwa ulaji huo hata mm nawaambia ukweli ingekuwa kuna visenti vya mmem vya kutosha ningenunua hadi gari tatizo vipo kidogo eti laki moja kwa robo mwaka, hata mtoa post akipewa ofis atakula tena zaid y Mr DEO
 
Back
Top Bottom