Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Afisa Habari wa Klabu ya Azam FC, Thabit Zakaria maarufu kama ZakaZakazi, amefungiwa kwa kipindi cha miezi mitatu (3) na kutozwa faini ya shilingi laki tano (500,000) kwa kosa la kushutumu Waamuzi wa mchezo kati ya Tanzania Prisons na Azam FC, kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari, mchezo ambao ulitamatika kwa Azam FC kukubali kichapo cha bao moja kwa bila dhidi ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.