DOKEZO Afisa Mikopo Chuo cha Mbeya University of Science and Technology (MUST) wapeni vijana stahiki yao (boom)

DOKEZO Afisa Mikopo Chuo cha Mbeya University of Science and Technology (MUST) wapeni vijana stahiki yao (boom)

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Mwaisa12

Senior Member
Joined
Jan 24, 2023
Posts
101
Reaction score
128
Habari wakuu, poleni na mjukumu,

Nimekuja kwenu na malalamiko na humu JF Kuna watu wa aina mbalimbali ambao wanaweza saidia watoto wetu.

Ofisi ya Mikopo chuo cha MUST mpaka sasa haijawaingizia baadhi wanafunzi wa mwaka wa kwanza pesa ya kujikimu (boom), pesa ambayo watoto wamesign mwezi wa kumi na mbili mpaka sasa hawajapewa, kweli? Na baadhi ya watoto wanatoka familia duni, huku wakitegemea pesa hiyo zaidi kujikimu.

Uongozi wa Wanafunzi, pamoja na Uongozi wa Chuo hautoi ushirikiano wa kutosha kwani wameegamia upande mmoja.

Hiyo ofisi imefatwa mara kadhaa kukumbushwa kuwawekea watoto pesa kwenye akaunti zao za benk, lakini wamekua wakitoa majibu ya kejeli kwamba wataweka wakijisikia na wasipangie ofisi kazi.

Je, hawa ofisi za mikopo wanakoswa utu kweli hata kwa Watoto wakimasikini, wanataka watoto wa kike wakafanye umalaya ndio walizike, ilihali pesa zilashatumwa akaunti ya chuo lakini wao hawataki kuweka.

Na kuna tetesi pesa za wanafunzi wao wanafanya biashara zao.

Serikali kupitia Wizara Ya Elimu mulika uozo MUST
 
Wamesaini halafu hela hawajapewa sasa inakuwaje unasaini kabla ya kupewa hyo hela
 
Ni Mambo ya ajabu kweli!! Swala lako linafanyiwa kazi mleta habari! Msalmie Sana msambichaka pamoja na Tweve
 
Wamesaini halafu hela hawajapewa sasa inakuwaje unasaini kabla ya kupewa hyo hela
First year Wana saini manual then ndio wanaenda kuingiziwa pesa.. Hawasain kwa mfumo wa vidole
 
Back
Top Bottom