Afisa Mtendaji wa mtaa wa Mbezi Msumi ashambuliwa hadi kufa ofisini kwake

Lol
 
Hata Hamza alipouwawa na polisi wananchi siku ile ile walichunguza na kusema alidhulumiwa madini, na wakalaumu polisi kwanini walimuua.
Ila yeye kuua askari 4 ilikuwa haina shida.

Nyerere hakutuachia utamaduni wa aina hii hata sijui tumeutoa wapi.Hivi sasa watumishi wa serikali yanapowafika mabaya watanzania tumekuwa watu wa kushangilia na kuwatetea wahalifu kuwa walichofanya ni sahihi.

Huyo mtendaji Kama angeweza kujihami na kufanikiwa kuwaua hao wahalifu leo tungesikia analaumiwa kwa kuchukua sheria mkononi, mara hawakumvamia amewaua kuficha ukweli juu ya dhuluma aliyowafanyia.

Hivi karibu Kuna tukio lilitokea la askari magereza wawili kutuhumiwa kubaka, hata hivyo ile ilikuwa ni tuhuma tu inaweza kuwa kulikuwa na makubaliano ambayo hayakufikiwa hivyo binti akaamua kusema alibakwa. Lakini wanachi walichunguza na kuhukumu siku hiyo hiyo ila tukio hilo angekuwa mlalamikaji ni askari watu wangekuwa upande wa mtuhumiwa.

Tuache chuki dhidi ya serikali na watumishi wa umma, haya mambo yanaanza kidogo kidogo tunaendelea kurithisha vizazi vyetu itafika hatua hatutaweza kuyarekebisha.

Tukumbuke uhalifu hauna macho.
 
Binadam ndo tulivyo huwa hatuishiwi Cha kusema ila kuvithibitisha tunavyo visema ndo huwa ni ngumu maana vingi n vya uongo na havna uthibitisho na hat ukweli ukidhihirishwa bado watu wataukataa na kuendelea kuamini hisia zao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…