KERO Afisa Rasilimali Watu TANESCO – Manyara anatumia cheo chake vibaya, Mamlaka za juu zichunguze

KERO Afisa Rasilimali Watu TANESCO – Manyara anatumia cheo chake vibaya, Mamlaka za juu zichunguze

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
NAOMBA UFICHUE UOVU DHIDI YA BI. NISILE MWAKALINGA - AFISA RASILIMALI WATU, TANESCO MKOA WA MANYARA

Mimi ni mtoa taarifa mwenye nia njema, naomba uchunguzi wa kina ufanyike dhidi ya Afisa Rasilimali Watu wa Mkoa wa Manyara, kwa madai yafuatayo:

1. Matumizi mabaya ya madaraka na kulipiza kisasi
Inadaiwa kuwa wafanyakazi wanaodhaniwa kuwa hawampendezi Afisa huyo huhamishwa mkoa bila sababu za msingi ikiwa ni wafanyakazi wa kudumu. Wafanyakazi wa muda husitishiwa mikataba bila kufuata mchakato wa haki na taratibu za ajira.

2. Ubaguzi na kuunda makundi kazini
Inadaiwa kuwa Afisa huyo anaendeshwa kwa mfumo wa upendeleo na kuunda makundi ya wafanyakazi wake, jambo linalodhoofisha usawa na mazingira ya haki kazini.

3. Mazingira ya hofu na ukimya wa kulazimishwa
Wafanyakazi wengi hawawezi kuripoti matatizo au kutoa maoni kwa hofu ya kupoteza ajira, kusitishiwa mkataba, au kuhamishwa mkoa bila sababu. Inadaiwa kuwa hali hii inajengewa nguvu na madai kuwa mume wa Afisa huyo ni mtu mwenye mamlaka katika vyombo vya usalama.

OMBI
Naomba uchunguzi wa kina, huru na wa haki ufanyike kuhusu madai haya. Ikiwa yatatibitika kuwa ya kweli, naomba hatua stahiki za kinidhamu na kiutawala zichukuliwe ili kurejesha haki, kulinda wafanyakazi, na kuhakikisha mazingira salama na ya kitaaluma kazini.
 
Kabla ya uchunguzi nyinyi mmechukua hatua gani za awali? Halafu nondo zako hazijashiba hii ni fichua maovu ilibidi umwage kila kitu hapa yaan umetupunja paragraph 3 tu kweli?.
 
Kabla ya uchunguzi nyinyi mmechukua hatua gani za awali? Halafu nondo zako hazijashiba hii ni fichua maovu ilibidi umwage kila kitu hapa yaan umetupunja paragraph 3 tu kweli?.
Kweli. Hatuoni majina wala mifano ya matukio halisi. Ajazie hivyo... Kwenye kila kila aya
 
Kwa utawala wa chura aka kizimkazi ndio kipao mbele chao watanganyika kuteseka kama kuzimu. Na bado kazi tunayo mbona tucpo jitetea.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Back
Top Bottom