Afisa Ustawi wa Jamii Ubungo: Watu kutoka kanda ya ziwa wanaongoza kutelekezwa na ndugu zao Stendi ya Magufuli

Afisa Ustawi wa Jamii Ubungo: Watu kutoka kanda ya ziwa wanaongoza kutelekezwa na ndugu zao Stendi ya Magufuli

Mtu anakusanya Viroba na ndala zake anakimbilia stendi anapanda Bus mpaka anafika Mlandizi ndio anakupigia sasa.

"Aloo? Ehh Ulimora Baba? Mwangaruka! eeh mimi Mjomba wako mtoto wa Bibi wa Simiyu, Kaka yake Baba Mkubwa, niko hapa MURANDIZI nakuja DAA, Nawomba unipokee hapo Sitendi Magufuri"

Hapo yupo na kitochi na elfu 1 mfukoni, simu yenyewe haina bundle wala chaji.

Hizi ni LAWAMA tunatafutiana.
Hahaaaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787]mjomba ndo unikimbiea[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Taarifa ni kwamba watu wengi wanaotoka mikoani kuja Dar es Salaam wamekuwa wakitelekezwa na ndugu zao stendi ya mabasi ya Magufuli, mamlaka za kituo hicho zimeamua kutangaza kwa kutumia Spika kuhusu ndugu ambao wanatelekezwa au wamekosa mwenyeji.


MIKOA INAYOONGOZA KUTELEKEZA NDUGU ZAO STENDI YA BASI
"Mikoa ya Kanda ya Ziwa yote tukianzia na Mara, Mwanza, Kagera (Bukoba), Geita (inaongoza (ndugu zao kuwatelekeza kituo cha Mabasi Magufuli wanapofika Jijini Dar es Salaam).

Pia kuna Mikoa ya Kigoma, Mbeya, Iringa, Morogoro na Dodoma na hatuna kitu cha kufanya zaidi ya kuelimisha jamii lakini pia tutaomba jamii iweze kuelewa kile ambacho tutakachokifundisha, elimu zinatolewa na tatizo lipo palepale" Naamini Nguve, Afisa ustawi wa Jamii Manispaa ya Ubungo.

Chanzo: Clouds TV

Pia soma - Watu wa Dar acheni kuwatelekeza ndugu zenu stendi


Hiyo nauli toka huko kanda za ziwa si angeongeza kuku akafuga akauza mayai?
 
Nakumbuka Kuna jamaa alijipatia mke pale mbez stend last year kutokana na hyohyo hali ya kutelekezwa na rafik yke waliopangana nae aje kutoka kijijini.,

Yule jamaa alienda mbezi kupokea mzgo wke akakutana na huyo Binti katika kuulizia ulizia ya yule Binti ikabidi jamaa ampe msaada wa kwenda nae ghetto coz ana dai hakuwa na ndugu zaid ya huyo rafik yke aliyemzimia simu hapa dar,, end the day jamaa mpka Leo yupo nae yule Binti kashakuwa mke.
 
Tatizo na nyie watu wa dar acheni kutupigia simu na kutuambia tuangalia facebook maisha mmeshatoboa kumbe unakaa stooo huna mbela wala nyuma.
Unapiga picha unagari sijui uko nje ya nyumba kali unaweka na ki caption Asante Mungu kumbe uko nje ya nyumba ya mwanaume mwenzako[emoji1787][emoji1787]
 
Naona wengi wanalalamika kuhusu kupewa taarifa kabla ya mtu kusafiri.Lakini ukweli ni kwamba mnaogopa ndugu zenu kwa sababu chakula cha watu 5 waishio mjini anakula mmoja aliyetoka kijijini.
Suluhisho waambieni waje na viroba vya mahindi na dagaa.
 
Naomba kujua mabasi ya mikoa hiyo yanafika sangapi?Ili nikimaliza kvant yangu hapa argentina manzense nikawinde mana naskia wanawake wa kanda ya ziwa wana matako laini kama supu ya mapupu.
 
Mimi sijaelewa, hivi hawa wanaotafuta ndugu zao ni watoto au ni watu wazima? kama ni watu wazima kwa nini wasiende moja kwa moja kwa ndugu zao ?
Ni watu wazima lakini washamba na wengi wao wanakuwa hawana nauli za kuwafikisha kwa ndugu zao. Pia, mjini ni vigumu kumtafuta ndugu yako kwa kumuelekeza kuwa unakaa mtaa fulani, akakupata (hata kwa kuuliza). Haiwezekani. Kumbuka watu wa mjini hatujuani kwa majina halisi.
 
Hili jambo lipo hata Dodoma na Morogoro, kuna binti aliishia mikononi mwa bodaboda na kupigwa mimba baada ya ndugu yake kupotea hewani pale Msamvu
Inaumiza sana
 
Sasa kama hao ndugu wanakimbilia mjini kishamba kwanini wasitelekezwe? Ndugu wa kijijini wana kawaida ya kuja mjini kwa kukurupuka. Mtu anasafiri kutoka kijijini bila kumtaarifu mwenyeji wake akifika Bus Terminal ndipo anakupigia simu umfuate wakati wewe hujajipanga kumlisha wala kumwandalia mahali pa kulala.

Tatizo mpaka sasa hivi watu wa mikoani wana ile mentality ya kizamani ya kusema: "Kaka yangu anafanya kazi TRA ngoja niende akanitafutie kazi hata ya kufagia hawezi kukosa". Wanadhani utaratibu wa kupeana kazi kizamani na kiholela bado upo. Hili ni tatizo.

Ipo haja kwa serikali kuwaelimisha watu wa kijijini namna nzuri ya kutembelea ndugu zao wa mjini Dar badala ya kukurupuka. Unakuta mtu anaishi na familia yake yote kwenye chumba kimoja cha kupanga, halafu mtu anakurupuka kimyakimya kutoka kijijini akifika Mbezi ndipo anakupigia umfuate. Umfuate uje kumlaza wapi na kumlisha nini?

Jamani tusiwatetee tu hawa jamaa bila kujua jinsi wanavyokurupuka kutoka huko kijijini bila mpango. Mimi hili tatizo liliwahi kunitokea. Nimekaa room sina hili wala lile napokea simu ngeni kutoka kwa ndugu yangu kwamba yupo Ubungo terminal nikamfuate. Kumbe alitumia simu ya abiria mwenzake hana hata simu. Ngoja nipate shida ya kuaga kazini na kumfuata huko Ubungo sasa! Nilikoma.

Baada ya kufika kwangu akakaa tu bila mpangokazi wowote. Fikiria wakati huo nakaa kwenye chumba kimoja kule Kinondoni mtaa wa Mgobanya. Na chumba hichohicho ndicho nakitumia mimi na demu wangu. Ilibidi sasa nianze kuingia gharama za kwenda kulipia pesa loji wakati nina room yangu. Na ghafla gharama za maisha zikapanda na kumbuka sikuwa nimejipanga kuwa na bajeti ya ziada ya kumlisha mtu wa ziada wala sikuwa na chumba cha ziada cha kumlaza.

Kwa hali kama hii unadhani kwanini wageni wasiendelee kutelekezwa? Tumechoka bhana, kama mbwai iwe mbwai!
Pole sana, wanapaswa wajifunze
 
Shida ndugu zetu wasukuma kupenda sifa . Yaani mtu akiwa na mjomba dar Kijiji kizima kinapata taabu mwishowe anaamua ajitose hukohuko Dar es salaam kwa Anko wake hata bila kuweka mambo sawa. Mwisho wa picha wanatelekezwa
 
Mtu anakusanya Viroba na ndala zake anakimbilia stendi anapanda Bus mpaka anafika Mlandizi ndio anakupigia sasa.

"Aloo? Ehh Ulimora Baba? Mwangaruka! eeh mimi Mjomba wako mtoto wa Bibi wa Simiyu, Kaka yake Baba Mkubwa, niko hapa MURANDIZI nakuja DAA, Nawomba unipokee hapo Sitendi Magufuri"

Hapo yupo na kitochi na elfu 1 mfukoni, simu yenyewe haina bundle wala chaji.

Hizi ni LAWAMA tunatafutiana.
Kwani mikoa ya Kanda ya ziwa ni wasukuma Tu ? Unaambiwa Kuna Kagera na Mara pia. Punguza chuki dhidi ya kabila kuu.
 
Back
Top Bottom