Afisa Utumishi Igunga avamiwa, ajeruhiwa kwa panga shingoni

Afisa Utumishi Igunga avamiwa, ajeruhiwa kwa panga shingoni

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Watu wasiojulikana wamemvamia na kumjeruhi kwa panga shingoni Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora, Mussa Abdallah.

Abdallah akiwa amejipumzisha nyumbani kwake Mtaa wa Mwayunge Kata ya Igunga mjini alipata mkasa huo baada ya kutoka kwenye kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauli ya Igunga, Machi 10, 2023.

Akizungumza kwa taabu akiwa Hospitali ya Wilaya ya Igunga ambako amelazwa kwa matibabu Afisa utumishi huyo alisema tukio hilo limetokea Machi 10, 2023 saa moja na nusu usiku.

Alisema akiwa nyumbani kwake amepumzika nje akiwa anaongea kwa simu ya mkononi alishitukia amekatwa panga shingoni na ndipo alikimbia kwa jirani yake ambaye ni Mganga Mkuu wa Wilaya ya Igunga aitwaye Lucia Kafumu kuomba msaada.

“Mimi nilikuwa nimejipumzisha nyumbani kwangu majira ya saa moja usiku baada ya kutoka katika kikao cha Baraza la Madiwani lakini ghafla nilivamiwa na kukatwa panga shingoni, nyinyi angalieni nilivyokatwa, nimeonewa sana lakini Mungu namshukuru kanisaidia sikutegemea kama nitaongea hivi," alisema huku akibubujikwa na machozi.

Afisa huyo alieleza kuwa huenda waharifu hao walikuwa wamejificha kwenye shamba la mahindi lililo jaribu na nyumba yake na kwamba watu hao baada ya kumjeruhi hawakuingia ndani kuchukua kitu chochote na hata simu aliyoidondosha wakati anakimbia hawakuichukua.

Naye Mganga Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Dk Lucia Kafumu amekiri kumpokea Afisa Utumishi huyo ambapo alisema walimpokea Machi 10, 2023 saa moja na nusu usiku akiwa amejeruhiwa shingoni upande wa kushoto.

"Baada ya kufikishwa katika hospitali yetu alipatiwa huduma ya kwanza kwenye jeraha hilo na hali yake inaendelea vizuri," amesema.

Nao baadhi ya Wananchi wa Igunga, Mrisho Hamisi, Mariam Jumbe, Hawa Willson, Idd Jackson wameeleza kushtushwa na kitendo hicho huku wakilitaka Jeshi la Polisi kuwasaka watu hao waliofanya unyama huo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi, Richard Abwao alithibitisha kutokea tukio hilo ambapo alisema jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi ili kubaini mtu au watu waliohusika na tukio hilo na watakapopatikana watafikishwa mahakamani.
 
Walitumwa kukata shingo nadhani hawakujua kwamba hawakuimaliza.
Kazini au mke wa mtu.
Wezi wangeondoka na kitu.
Jamaa anaonekana yupo vizuri ,

Walijaribu kupiga madawa kwenye kiti chake...hola....kwenye misosi na Maji kunywa ...hola...

Mganga akawaambia nguvu zake zipo shingoni....na tena kama mkitaka kuziondoa...msipite mbele yake...pitieni mgongoni kwake...
 
Jamaa anaonekana yupo vizuri ,

Walijaribu kupiga madawa kwenye kiti chake...hola....kwenye misosi na Maji kunywa ...hola...

Mganga akawaambia nguvu zake zipo shingoni....na tena kama mkitaka kuziondoa...msipite mbele yake...pitieni mgongoni kwake...
Atakua aliwatesa kwa namna moja au nyingine.
 
Atakua aliwatesa kwa namna moja au nyingine.
Mimi jamaa walini time...wakaniwekea maudambwi kwenye kiti...nilikuaga mtumishi mzuri sana....nikajikuta naichukia Kazi...kisha nikasepa.....nikafukuzwa na Kazi. Akili zikaja baada ya 7 years....nikaanza kushangaa how I left the job.

Dah huko ma halmashauri sio poa kabisa!!!


So huyo wa Igunga...huenda ikawa ni wivu, chuki, fitina,

Au mapenzi?

Note:- kwangu ilikua ni kuhudumia watu bure bila kupokea 10% , jamaa wa Idarani wakaanza kumind.

Na pia, nilikua napiga Kazi kwà Bidii sana mpaka weekends....wakuu wa IDARA zote wakawa wananipenda sana mpaka Mkurugenzi. Nikapewa na kiusafiri cha pikipiki...., , Jealous zikazidi. Nikapigwa bonge la juju....daah sio poa yani.
 
Back
Top Bottom