DOKEZO Afisa utumishi, PSSF wachezea mfumo na kumstaafisha mtumishi kabla ya muda, alilipwa Milioni 72, akapokea Milioni 2 tu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Aseee! Ni ushetani mkubwa sana.
 
[emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419]

Alafu ela za zambi hvyo anatamba nazo na kujiona yeye mpambanaji wengine tunabak kutumia kichwa jamaa mbona anatoboa.
Kumbe huwa unapoteza muda kuwaza watu? Utakufa braza!

Hata wasioiba wanaroga balaa, kawaangalie Wakinga pale Kariakoo wanavyoroga...

Shauri yako
 
Hao Bank wanamkopeshaje mtu anayekalibia kustaafu? Lets say amebakiza miaka mi5 je kwa calculations zao kwa huo muda wa miaka 5 hiyo hela ingerudi? Ukizingatia AJIRA yake ndio dhamana ya Mkopo?

Kuna kitu sijakielewa.. je huy mtumishi alikopa kias gani..? Muda aliokopa ni upi? Na kama alikopa je terms za kurudisha mkopo upoje..? Haiwezekan mkopo wa miaka 7 wewe uchukue hela yako ndani ya miaka miwili...


Haya turud ktk kanuni na taratibu za kibenk.. je ni sahihi kunyofoa hela zote hizo bila kuruhusiwa na mwenye account..

Je kiwango cha kurudisha mkopo kwa mkupuo ndio kipo hivyo?

Kuna maswali mengi kwa uelewa wangu mdogo nashindwa kudadavua hii ishu.
 
Hapo PSSSF kuanzia makao makuu Dodoma pameoza.

Hicho kitengo cha Huduma kwa wateja wanatumia hiyo ofisi kutapeli wastaafu wengi tu.

Kinachofanyika ni pale mstaafu akiwasiliana nao kuomba ufafanuzi kwa mawasiliono ya ofisi wao humpigia kwa namba zao binafsi na kifuatacho ITV ni kwamba hupotoshwa na kutapeliwa.

Either wanashirikiana na watu wa nje ya PSSSF kwa kuwapatia taarifa za wazee hao ili wapigwe au wenyewe kabisa wanasimamia show.

RB zipo kila mahali ila cha kushangaza hakuna hatua za maana zimechukuliwa.

Polisi kitengo cha cyber kingebinafsishwa wakapewa watu competent.
 
Mimi uncle wangu aliyekuwa Afisa Mwandamizi EAC walimtengenezea cheti feki cha kifo na wakakomba mafao yake na pensheni zote 100%.

Siku alipozuka kuzichukuwa mwaka 2012 baada ya Mahakama ya Tz kuamuru walipwe, wale staffs wa huduma kwa mteja baada ya kuangalia kwenye mfumo wa tarakilishi (computer) wakapiga ukunga/yowe/nduru kuwaita staffs wenzao eti wamezukiwa na mzimu.

Walipofika staffs hao na kuuliza mzimu upi, wakamwonyesha huyo hapo (yaani uncle wangu).

Uncle alipouliza ni kwa vipi wamnyanyapae kiwango hicho kwa kumuita mzimu wakati amekuja kudai haki zake?

Wakasema mfumo unaonyesha wewe ni marehemu tangu mwaka 1985 na kivuli cha cheti cha kifo hiki hapa kwenye tarakilishi na mafao uliishachukuwa ushahidi huu hapa na mwenzi wako alichukuwa nusu pensheni hadi 1986.

Wale staffs walioitwa kushuhudia mzimu wakayeyuka, uncle puuuuu.... chini, pepewa pepewa pale na walinzi, fahamu ziliporudi akaacha laana ya karne (kama serikali inalaanika sijui!?) na kuondoka hapo Hazina Makao Makuu hadi leo yuko hai Kijijini kama EL kule Peninsular; na akasusa kabisa kurudi Hazina.

Aina hii ya watumishi ndiyo wamejaa serikalini na ndiyo watafanya models kama za akina Makonda zisiishe nchi hii, zitakuja na kutoweka na kurudi tena na kutoweka tena na kurudi...
 
Kama hakuchukua yeye kwanini asidai haki yake .hata bank Hela huwa inaibwa Ila uchumguzi inafanyikia mhusika anarudishiwa
 
Kukopa Kwa mstafu ni kawaida....hata aliyestafu anaruhisiwa kukopa against a pension
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…