Bezecky
JF-Expert Member
- Apr 28, 2024
- 494
- 897
WAKATI MAJIMBO NA MIKOA HAMPATI HATA LAKI MOJA YA KUWASAIDIA KWENYE KAMPEINI KUJENGA CHAMA, MAKAO MAKUU TUMEGAWANA ZAIDI YA MILIONI MIA NNE KUTOKA KWENYE RUZUKU
Nawasalimu wakubwa Viongozi na wanachama, Leo nataka niwafumbue macho kidogo juu ya Ruzuku Yenu ambayo inatokana na mchango wa kila mwanachama anayeshiriki kutafuta kura za ubunge na urais
Iko hivi;
Baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2020 na Uamuzi wa Kamati Kuu kutokuutambua uchaguzi ule na vyote vilivyotokana na uchaguzi ule, tuliamua kususia Ruzuku. Kwa vile watumishi wa Chama na Kanda wanalipwa hivyo kukosa Ruzuku Chama kiliamua kufunga makao makuu pamoja na kanda.
Tulifanya Kikao Ofisini Makao Makuu, na kupewa taarifa ya kuwa kuanzia sasa Chama hakitakuwa na mfanyakazi hata mmoja, hivyo yeyote atakayejisikia kuendelea kujitolea aendelee na yule ambaye hawezi kujitolea akae Nyumbani, Sababu iliyopelekea uamzi huo ni ukosefu wa Ruzuku.
Mimi niliamua kufanya mambo mawili;
1. Nilikubali kuendelea kujitolea bila malipo yoyote yale kwani mimi niliunga mkono hatua za kutokuchukua ruzuku
2. Niandika mpango kazi ambao nilielezea namna Chama kinaweza kupata fedha ya kujiendesha. Mpango huo ulilenga kuingiza milioni mia mbili na arobaini kila mwezi. ( Kwa bahati mbaya haukufanyiwa kazi wala kupewa kipaumbele)
Baada ya kikao hicho, Watumishi waliacha kwenda ofisini, tulibaki wachache sana ambao tuliendelea kujitolea naweza kuwataja kwa majina ila naomba kuyaifadhi.
Kwa kibindi hicho kuanzia November 2020 hadi May 2021, kwa upande wa Viongozi wa wakuu (Secretariat) aliyekuwa anaonekana ofisini mara kwa mara ni mmoja tu Wengine wote walichimba.
Ilipofika May 25, 2021 wote wakarudi kwa sababu ya uzinduzi wa Chadema Digital na Operation Haki ambayo ingeambatana na posho za Operation. Tulizunguka nchi nzima , Mimi binafsi nilizunguka kila sehemu tulikuwa tunalipwa pesa nzuri tu. ( Operation Haki ni Pigo ltakuja)
Digital watu wakaipokea pesa ikaaza kuingia, kwa usiri mkubwa watu kadhaa wakajitenga na kuanza kulipwa upya posho ya kila mwezi. Mimi nikatengwa na hili nisijue nikaambiwe nikiwa nafika ofisini kufanya kazi nisisaini kwenye kitabu cha watendaji badala yake nisaini kitabu cha wageni. Nikajua tayari, hela imeingia. Nikakubali kutokusaini kitabu chochote ila ofisini nitakuwepo na kazi za Chama nitafanya.
Kipindi hicho nikaamua kwenda majimboni kufanya kazi zaidi, nikatembelea majimbo kwa gharama za viongozi wa majimbo . Kwa haraka nilitembelea Singida, Rombo, Mlimba, Morogoro Mjini, Songea Mjini, Tanga mjini, Muheza, Dar es Salaam N.k kote nikaenda kuwajengea watu uwezo, kutengeneza watalaamu wa usajili kupitia mifumo, kuwapa printer na kuwafundisha namna ya kutumia mifumo kuzalisha kadi, na kuelekeza namna ya kutumia mifumo ya Chama. Hapo Ruzuku Bado haijachuliwa ila wanajilipa pesa ambayo mimi na wengine wachache (HQ) tunaizalisha kwa kufanya kazi, wanaozalisha fedha ya Digital husasani mimi Sipo kwenye Hiyo Posho yao, ambao hawaingizi chochote wanajilipa. Wakasahau hata majimbo wanazalisha lakini hawalipwi (Ili la Chadema Digital kuna Pigo litakuja)
Baadhi ya watendaji wakawa wananiuliza mbona haulipwi si umbane Katibu Mkuu akulipe? Mbona wewe ndo unazalisha fedha? Nikawaambia viongozi wa majimbo wilaya nao si wanazalisha kwani wanalipwa? Nami nifanya kazi HQ naishi kama wengine kwenye majimbo, Ninauwezo wa kupata hicho wanachojilipa wakitaka watatoa wasipotaka tutajenga Chama. Naibu Bara alimbana sana Katibu Mkuu ila alizidiwa.
Kibembe kikaanza baada ya Ruzuku Kuchukuliwa!
Naomba tega sikio, utulie usome na uelewe. Secretariat ilipoona Ruzuku imeingia hatua ya kwanza waliwaza kujilipa wao then hatua ya pili iwe ni kwenda Field kujenga Chama. Wakajaribu kujigawia vipande vya fedha wakakwama kwenye vikao vya Kamati Kuu. Kwasababu wajumbe wachache wa Kamati Kuu walikaza sana. Wakarudi tena mara ya pili bado wajumbe wakagoma kuwaruhusu, wakaamua kufanya Robbing (Hapa kuna mchezo mchafu ulifanyika) kwa Mwenyekiti wa Taifa wakakubaliana na wakarudi mara ya tatu Kamati Kuu na wakakubaliwa wajilipe. Wajumbe waliokuwa wanakataa mambo ya kujilipa Ruzuku ni hawa hapa waulize John Heche, Peter Msigwa, Gaston Garubindi, Ezekia Wenje, Godbless Lema ndo walikuwa wanapinga kwa nguvu zote, Wajumbe hawa walijitengenezea ugomvi mkubwa na Secretariat na mkakati wa kuhakikisha hawarudi kwenye CC ulianza kusukwa. ( Hii ya Wajumbe wa CC nitaileta kama Pigo linalojitegemea )
Kiasi gani walijilipa
Ili ujue kiwango gani walijilipa, inabidi ujue hawa watumishi wenu mishahara yao kwa mwezi ni Sh. Ngapi.
1. Manaibu 3.5 M kwa Mwezi
2. Wakurugenzi 2.5M kwa mwezi
3. Watendaji wengine wako kati ya 600,000 hadi 1.5M
Sasa, ili wajilipe Ruzuku ilitengenezwa Fomula yankula hizo hela,
Moja, lilibuniwa jina la mgao wakaliita " Hardship Allowance" yaani malipo ya mazingira magumu waliopitia
Mbili, kila mmoja alitakiwa kujilipa mshahara wake kwa miezi 12. Yaani kama Mshahara ni milioni moja maana yake alilipwa milioni moja mara 12. Nadhani unaninelewa na unaweza kufanya hesabu ukajua kila mmoja alilipwa sh ngapi na ukapata hesabu ni milioni Ngapi zilitumika kujilipa mara tu baada ya Ruzuku kutoka.
Waliojilipa ni Secretariat, Makatibu wa Kanda ( Japo walipigwa pia) na watumishi wachache ambao waliona wanawafaa majina ninayo. Wakati haya yanafanyika, wafanyakazi wa chini waliowengi waliondolewa hawakupewa ( Hili nalo ni pigo Lingine)
Sasa, Mimi waga ni mtata na wanajua utata wangu sikupewa mgao, nikawafuata nakasema tulikubaliana Ruzuku hatuchukui, mmechukua, tulikubaliana watumishi wote wameondolewa kwa sababu hakuna ruzuku sasa mbona ruzuku mmechukua na hamjawaita? Nikasema hata mimi ambaye ndo nipo ofisini siku zote, nafanya kazi, silipwi wanalipwa wengine ambao hata ofisini hawaji na hii Ya Ruzuku mnaniweka pembeni? Nikawaambia Hii Ruzuku mtanilipa kama mlivyojilipa ama mnataka au hamtaki mtalipa. Nipo hapa hapa naona mchezo alafu niwaache! Nikamuandia Waraka Katibu Mkuu nikimtaka anilipe sawa sawa na alivyowalipa wengine. Katibu Mkuu akanilipa. Mimi nikapewa Milioni Tatu kwa kuandikiwa Cheque. Baada ya kuichukua, nikamwambia hii haifiki hata robo ya kile unatakiwa ulipe yote haya walikuwa wanagoma wakijua nitapata ushahidi.
Ndugu yangu mpiga kura naomba Jipe muda utafakali na ufanye jambo sahihi tunakoelekea kutafuta Mwenyekiti wa Chama Taifa, ambaye ataunda Secretariat yake mpya;
1. Fikilia Mtu anayewaza kujilipa milioni 12, 25, 30, 50 n.k na mwisho wa mwezi analipwa vile vile alafu Kamati Tendaji ya Kanda hamna hiyo Taarifa, Mkoa, wilaya, Jimbo n.k hata 500,000 hujawai kuipata. Fikilia alafu fanya maamuzi.
2. Fikilia Kwa nini Enzi za Dr. SLAA pamoja na Ruzuku kuwa ndogo baadhi ya majimbo kama sio yote mlikuwa mnapata Ruzuku. Kwanini sasa hivi hampati?
3. Fikilia Chama ambacho kinataka kuchukua dola, tunaambiana Komaa Kamanda na kweli tunakomaa alafu nyuma ya pazia watu wanachukua fedha nyingi kiasi hizo, Mishahara mikubwa kama hiyo. Je? Hawa wanapambania Chama? Hawa nadhani ndo wale walimuambia Mwl. Nyerere usiondoke hii nchi bado changa.
4. Fikilia watu ambao wanaweza kubuni jina zuri la mgao wa Ruzuku na kuliita "HARDSHIP ALLOWANCE". Hivi mazingira magumu yalikuwa HQ peke yake?
5. Waulizeni Hao wanaosema walienda kimshawishi Mwamba, je? Kwenye Mkoa walipewa Hardship Allowance? Kama walipewa nyie viongozi wa majimbo wilaya mlipata? Wanachama je wanajua haya?
5. Waulizeni wajumbe wa Kamati Kuu, kama ninadanganya. Mimi ni Shahidi nipewa.
6. Muombeni Katibu Mkuu atoke awape majibu. Muulize kama nasema uongo, muulize kama sikusema ndani wakanipuuza nikawaambia nitasema kwa wenye Chama.
Sasa ni Muda wa kuwaambia hiyo Hardship Allowance itafika lini jimboni kwako? Kama hawana majibu, Tuletee Mtu Sahihi wa Kutubadilishia Secretariat naye Sio Mwingine Ni Tundu Lissu. Mwenyekiti Mbowe mimi nampenda lakini hawezi kuwafanya kitu chochote, wajumbe wa CC baadhi walijaribu kufanya mabadiliko hawakuweza Chairman aliwalinda.
Chukua hatua, Nusuru Chama
Remigius Constantine HQ