Afisa wa GSU apoteza bastola wakati wa mazishi ya Raila Odinga, Bondo

Afisa wa GSU apoteza bastola wakati wa mazishi ya Raila Odinga, Bondo

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Afisa mmoja wa Kikosi cha GSU aliyeambatana na msafara wa ulinzi wa Gavana wa Kakamega, Fernandes Barasa, amethibitisha kupoteza bastola yake wakati wa mazishi ya Waziri Mkuu wa zamani, Raila Odinga, yaliyofanyika katika eneo la Bondo, Kaunti ya Siaya Oktoba 19, 2025

Kwa mujibu wa maelezo ya afisa huyo, vijana waliokuwa akiwashuku walimvamia kwa ghafla wakati jeneza la marehemu likipelekwa kwa maziko katika eneo la Kang’o KaJaramogi, baada ya ibada ya mazishi iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Jaramogi Oginga Odinga (JOOUST)

Vijana hao walifanikiwa kunyakua bastola iliyokuwa na risasi 15, ambayo ilikuwa imefungwa kiunoni mwa afisa huyo, kisha wakatoroka kwa kasi wakitawanyika miongoni mwa umati mkubwa wa waombolezaji.

Tukio hilo liliripotiwa kutokea majira ya saa 10:30 jioni siku ya Jumapili

Ripoti za polisi zinaonyesha kuwa mamia ya waombolezaji pia walipoteza mali zao, ikiwemo simu za mkononi, pochi, na nguo kama koti na kofia ambazo zilikuwa zimetoweka bila kutambulika.

Maafisa wa usalama wameanzisha uchunguzi kubaini waliohusika katika tukio hilo na kuhakikisha bastola hiyo inapatikana

1761031250735.png


Source: buzzroomKenya
 
Ujanja ukizidi unakua ujinga.
Huyo jamaa atapatikana, atachomwa na vijana wenzake.
Maisha yake yatakua mbaya sana
 
Back
Top Bottom