Afisa wa Jeshi la wanamaji nchini Nigeria amzuia waziri kuingia kwenye eneo la ardhi lenye mgogoro jijini Abuja

Afisa wa Jeshi la wanamaji nchini Nigeria amzuia waziri kuingia kwenye eneo la ardhi lenye mgogoro jijini Abuja

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Vijana sasa wanakiwasha kila sehemu, hakuna uonevu tena! Huyu waziri amejikuta anafoka hadi mishipa ya mwili mzima imemsimama lakini kamanda mwenye anajibu kwa utulivu hapa uingiii kabisa!
=====================

Afisa kijana wa jeshi la wanamaji nchini Nigeria amepokea sifa kubwa kwenye mitandao ya kijamii baada ya kubaki na utulivu na kusimama kidete alipomzuia Waziri wa Eneo la Mji Mkuu wa Shirikisho (FCT), Federal Capital Territory, Nyesom Wike, kuingia kwenye eneo la ardhi lenye mgogoro jijini Abuja – tukio lililonaswa kwenye video ambayo sasa imeenea mtandaoni kwa mamilioni ya watazamaji.

Tukio hilo lilitokea Jumanne, Novemba 11, 2025, wakati Luteni A.M. Yerima, aliyekuwa akiongoza kikosi cha wanajeshi waliokuwa na silaha, alipomzuia Waziri Wike kuingia katika eneo la Mabushi, akieleza kuwa alikuwa anatekeleza amri za wakuu wake.

 
Back
Top Bottom