Tetesi: Afisa wa mgodi wa GGM uliopo Geita aliwa na mamba kisiwa cha Rubondo

Tetesi: Afisa wa mgodi wa GGM uliopo Geita aliwa na mamba kisiwa cha Rubondo

KILYA BIYE

Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
52
Reaction score
12
Habari zenu wadau,

Kuna habari inasambaa kuwa, kuna maafisa wa mgodi wa GGM walienda kula maisha huko Rubondo siku ya jana Jumamosi, bahati mbaya wakiwa wanaendelea kutumia vinywaji vyao,mmoja wao akateleza na kudumbukia kwenye maji na hapo akakutana na mamba uso kwa uso na hivyo kupelekwa na mamba huyo.

Kwa wasiojua ni kwamba Rubondo ni kisiwa ambacho kipo ziwa Victoria, pia ni hifadhi ya taifa.

Swali langu ni kutaka kujua kama habari hiyo ni ya kweli, pili kama ni kweli , ina maana hapo kisiwa cha Rubondo ambayo ni hifadhi ya taifa hakuna usalama kwa watalii au kuna mkakati gani wa kulinda watalii wanaofika hapo?
 
Aisee kwani hakupewa tahadhar kuhusu hilo eneo au ndio deal done??
 
Ni kweli Mkuu, inasemekana alikuwa mkuda anaharibu kazi za wenzake Kwa kujifanya yeye ni Mungu mtoa riziki.
Watu wakaingia front ndo maana yamemkuta.
Mkuu fafanua tafadhali
 
Ni kweli Mkuu, inasemekana alikuwa mkuda anaharibu kazi za wenzake Kwa kujifanya yeye ni Mungu mtoa riziki.
Watu wakaingia front ndo maana yamemkuta.
Duuuh kwa nn na huyu wacha waisome namba aisende kupumzika huko....
 
Haijafahamika vizuri kilichotokea lakini timu ya wapiga mbizi wapo ndani ya ziwa victoria eneo la tukio wanaendelea kumtafuta bado hajapatikana.
 
Ni kweli Mkuu, inasemekana alikuwa mkuda anaharibu kazi za wenzake Kwa kujifanya yeye ni Mungu mtoa riziki. Watu wakaingia front ndo maana yamemkuta.
Kwa hio walimsukumiza kwenye maji? Au una maana gani?
 
Haijafahamika vizuri kilichotokea lakini timu ya wapiga mbizi wapo ndani ya ziwa victoria eneo la tukio wanaendelea kumtafuta bado hajapatikana.
Sasa kama mamba keshamfanya kitoweo atapatika vipi mkuu?
 
Ni kweli Mkuu, inasemekana alikuwa mkuda anaharibu kazi za wenzake Kwa kujifanya yeye ni Mungu mtoa riziki. Watu wakaingia front ndo maana yamemkuta.

Ama kweli teknolojia inakuwa kwa kasi yaani walimsukuma kwenye maji kwa remote
 
Kwa hiyo death certificate itaandikwa kaliwa na mamba?au wataandika ajali.
 
Ni kweli Mkuu, inasemekana alikuwa mkuda anaharibu kazi za wenzake Kwa kujifanya yeye ni Mungu mtoa riziki. Watu wakaingia front ndo maana yamemkuta.
Jamani maana haita tuacha..usiue nidhambi
 
Back
Top Bottom