Africa Climate Summit 2023: Afrika hupoteza 5%-15% ya pato la ndani kila Mwaka kutokana na athari za Mabadiliko ya Tabianchi

Africa Climate Summit 2023: Afrika hupoteza 5%-15% ya pato la ndani kila Mwaka kutokana na athari za Mabadiliko ya Tabianchi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Rais wa Kenya William Ruto amesema Mabadiliko ya Tabianchi yanatafuna maendeleo ya kiuchumi ya Afrika na ni wakati wa kuwa na mazungumzo ya kimataifa kuhusu kodi itakayotozwa wachafuzi wa mazingira.

Kwa mujibu wa rais Ruto, bara linalokua kwa kasi la Afrika lenye wakazi bilioni 1.3 linapoteza asilimia 5 hadi 15 ya ukuaji wa pato lake jumla la ndani kila mwaka kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi, akiutaja upotevu huu kuwa chanzo cha mfadhaiko mkubwa katika bara hilo lenye utajiri mkubwa wa rasilimali na ambalo linachangia kidogo sana kwenye ongezeko la joto la dunia.

Hotuba za ufunguzi wa mkutano huo zimejumuisha wito wa wazi wa kufanya mageuzi ya mifumo ya fedha duniani ambayo imeaacha mataifa ya Afrika yakilipa takriban mara tano zaidi ya kwenye pesa za mkopo kuliko mengine, na hivyo kuzidisha mzozo wa madeni kwa wengi. Waziri wa Mazingira wa Kenya Soipan Tuya, amesema Afrika ina zaidi ya nchi 30 zenye madeni zaidi duniani.

Mjumbe wa serikali ya Marekani kuhusu tabianchi, John Kerry, amekiri juu ya deni kubwa na lisilo la haki, na kuongeza pia kwamba mataifa 17 kati ya 20 duniani yalioathiriwa zaidi na mabadiliko ya tabianchi yako barani Afrika, wakati mataifa 20 tajiri zaidi duniani, likiwemo lake, yanazalisha asilimia 80 ya hewa ukaa duniani ambayo inasababisha mabadiliko ya hali ya hewa.

Ruto alisema nchi 54 za Afrika "lazima zikumbatia haraka teknolojia rafiki kwa mazingira kabla ya kukuza viwanda na si kinyume chake, tofauti na anasa yaliokuwa nayo mataifa tajiri kufanya hivyo."

Kubadilisha uchumi wa Afrika katika mwelekeo wa kijani "ndio njia inayowezekana zaidi, ya haki na yenye ufanisi ya kufikia ulimwengu wa kiwango sifuri cha gesi ya ukaa ifikapo mwaka 2050," alisema.

Ufadhili wa tabianchi ni muhimu, wasemaji walisema, huku ahadi ya mataifa tajiri ya dola bilioni 100 kwa mwaka katika ufadhili wa hali ya hewa kwa nchi zinazoendelea ikiwa bado haijatekelezwa. Ruto alisema tamko la mkutano huo "litahimiza" kila mtu kutimiza ahadi zao.

DW Swahili
 
Back
Top Bottom