Africa haiwezi kujlisha kama inalima mazao kama mahindi na mpunga badala ya Ulezi na Mtama.

Africa haiwezi kujlisha kama inalima mazao kama mahindi na mpunga badala ya Ulezi na Mtama.

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Habarini ya sherehe za uhuru? Mtu ambaye hawezi kujilisha hawezi kuwa huru.

Kila mazao ya chakula kuna hali ya hewa inafaa kuyalima. Mahindi yalikuwa yanastawi kwenye temperate climates huko America, yaani kusiko na baridi kali ya barafu lakini kuna mvua nyingi, ngano nayo hivyohivyo. Mchele unataka maeneo chepechepe na joto, yaani maji mengi sana.

Sasa, katika mabara yote Africa inaongoza kwa joto na ukame ukifuatiwa na Australia. Na nafaka ya asili iliyokua huko ni ulezi na mtama. Hizi nafaka zinastahimili joto kali na ukame. Na kitu kama Ulezi unaweza kuvuna hata mara mbili kwa mpando mmoja.

Sasa bahati mbaya kwa kuiga wakoloni tumeanza kupanda mazao ambayo yanastawi sehemu chache sana za bara letu. Utaona mahindi na ngano vinasitawi vizuri kwenye hali za baridi na mvua nyingi, sehemu ambazo ni chache sana nchini na kwenye bara letu. Mpunga utaukuta kwenye mabonde chepechepe ambayo nayo ni machache sana.

Ili tuwe huru dhidi ya njaa inatupaswa kurudia kulima mazao ya asili ya bara letu. Ulezi na Mtama. Mazao yanayositawi karibu kila kona ya bara letu. Hatutaishinda njaa, au kwa kulima mahindi na mchele. Ulezi
1670594916083.png

1670594959491.png

1670594990661.png
 
Ngano, mtama ( mweupe na mwekundu) , muhogo, uwele au ulezi, viazi vikuu, viazi vitamu ni mazao yanayostawi sana Maeneo mengi afrika
 
Lakini pia maeneo mengi ya Afrika Bangi inastawi sana tungeweza kuilima kwa kiasi kikubwa na kupata bidhaa nyingi sana kama mafuta, nguo, chocolate, na kadhalika
 
Ngano, mtama ( mweupe na mwekundu) , muhogo, uwele au ulezi, viazi vikuu, viazi vitamu ni mazao yanayostawi sana Maeneo mengi afrika
Si maeneo mengi. Mfano hiyo ngano utaikuta Mbeya na Njombe na maeneo machache yenye temperate climates. Sehemu nyingi za savana, kama sehemu kubwa ya Tanzania mazao hayo hayastawi.
 
Lakini pia maeneo mengi ya Afrika Bangi inastawi sana tungeweza kuilima kwa kiasi kikubwa na kupata bidhaa nyingi sana kama mafuta, nguo, chocolate, na kadhalika
Bangi quality inahitaji uwanda wa juu na mvua ya kutosha.
 
Back
Top Bottom