Kama ulikua humjui vizuri Patric Lumumba wacha nikufahamishe;-
Patrice Lumumba alizaliwa tarehe 2/7/1925 na François Tolenga Otetshima, na Julienne Wamato Lomendja, ambao walikuwa wafugaji katika kijiji cha Katakokombe katika wa Mkoa wa Kasai katka jimbo la Kanyalwaunga. alikuwa mwanachama wa Kikundi cha nidhamujina harisi la Patrice Lumumba lilikuwa Élias Okit'Asombo.
Jina hili likiwa na maana "heir of the cursed"ambalo lilitokana na neno la Tetela ambayo ni miongoni mwa makabila ya congo okitá/okitɔ́ ('Mrithi') na asombó ('cursed or bewitched people who will die quickly').
Alikuwa na kaka zake watatu ambao ni
(Charles Lokolonga, Émile Kalema, na Louis Onema Pene Lumumba) na ndugu yao wa karibu (Tolenga Jean).
Alilelewa katika makuzi ya familia ya Kikatoliki alisoma katika shule ya msingi ya Shule ya Protestant , Shule ambayo ilikuwa inamilikiwa na wamisionari wa Kanisa Katoriki, na baadaye alipata mafunzo katika chuo kimoja cha serikali , alijishindia kozi mbalimbali na kisha kuajiliwa, alipata kazi katika mji wa Léopoldville ambao kwa sasa unajulikana kwa jina la Kinshasa) na baadaye katika mji wa Stanleyville ambao nao kwa sasa unajulikana kwa jina laKisangani ambapo alifanya kazi kama kalani wa posta na pia alikuwa akifanya kazi ya uuzaji wa bia kwa wasafiri.
Mnamo mwaka 1951 alimuoa Pauline Opangu . Mwaka 1955 Lumumba alipanda cheo na kuwa Cercles wa mji wa Stanleyville na baadaye alijiunga na chama cha Liberal Party of Belgium, ambapo alifanya kazi ya uharariri na usambazaji wa kijarida cha Chama cha Kiliberali cha Ubeljiji.
Na baadaye alifanya ziara ya mafunzo ya wiki tatu nchini Ubeljiji,mwaka 1956 alikamatwa na kushitakiwa kosa la ubadhilifu na kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kifungo cha nje na kasha baadaye wakili wa baada ya wakili wa kibaljiji kuthibitisha kwamba Lumumba amesharejesha zile fedha aliachiliwa huru mnamo mapemwaka 1956.
Na baada ya kuachiliwa kwake alisaidiwa na kuanzisha chama chamaw:Mouvement national congolais (MNC) mnamo. Mwaka 1958, alichaguliwa kuwa Rais wa chama hicho.
Mnamo mwaka 1958 mwezi wa Desemba Lumumba na wenzake walikiwakilisha chama chao katika mkutano wa All-African Peoples' Conference Baraza la watu wote wa Africa mjini Accra, Ghana, katika mkutano huo wa Desemba waPan-African uliokuwa chini ya Rais wa Ghana hayati Kwame Nkrumah , Ndg Lumumba ambaye alionekana kuongea lugha nyingi zikiwemo za Tetela, French, Lingala, kiswahili, na Tshiluba alijitambulisha zaidi dhidi ya imani yake kwa bara la afrika .
[emoji117]Uongozi wa MNC.[emoji288]
Mnamo mwezi wa octoba, mwaka 1959, Lumumba, kama kiongozi wa chama cha MNC, alikamatwa kwa kosa la kuchochea vurugu zakupinga serikali ya kikoloni katika mji wa Stanleyville ambapo watu takriban 30 waliuawa na yeye alihukumiwa kwenda jela kwa miezi sita.
Mnamo tarehe 18 ya mwezi January 1960 ambayo ilikuwa siku ya majaribo na hapohapo katika siku ya kwanza ya mkutano wa kuzungumzia hatma ya nchi ya kidemokrasia ya Congo itakumbukwa kwamba licha ya Lumumba kuwa jela katika kipindi hicho cha chake cha MNC kilifanikiwa kuwashawishi wananchi kwenye uchaguzi uliofanyika mwezi Decemba na kushinda katika jamhuri ya Congo.
Kutokana na nguvu ya umma iliyokuwa ikifanywa na wananchi wa Congo dhidi ya kuachiliwa kwa Lumumba kutoka kila kona, aliachiliwa na kuruhusiwa kuhudhuria katika mkutano wa Brussels. Mkutano huo ulifikia kilele tarehe 27, June 1960 kwa azimio la uhuru wan chi ya Congo na kupanga uchaguzi tarehe 30 ya mwaka huo huo wa 1960 Uchaguzi Mkuu wa Congo 11–25 May 1960.
Lumumba na chama chake cha MNC walipata ushindi uliowawezesha kuunda serikali kwa tangazo la tarehe 23 June 1960 na Patrice Lumumba anapata cheo cha uwaziri mkuu akiwa na umri wa miaka 34 na Joseph Kasa-Vubu akiwa ndie Rais wake wa kwanza.
Kwa mujibu wa katiba ya Congo mnamo tarehe 24 June Serikali ilipitisha kura ya kijasiri ambayo iliamuliwa na baraza la maseneta kuwa kwamba tarehe 24 iwe ni siku ya ya kuadhimisha uhuru wa Congo.
Maadhimisho ya uhuru wa Congo kwa mra ya kwanza yalifanyika mnamo tarehe 30 June 1960 ambapo maadhimisho hayo yalihudhuriwa pia na Mfarme Baudouin wa Ubeljiji pamoja na vyombo mbalimbali vya habari kutoka nchi za nje.
Lumumba alitoa hotuba yake kama Waziri mkuu katika nchi huru japo yeye alikuwa ameenguliwa katika ratiba ya shughuli hiyo.
Hotuba ya Mfalme wa Ubeljiji Mfalme Baudouin alihutubia kwa kutukuza utawala wa kikoloni, huku akilingania fikra za mjombae ambae alikuwa mfalme wa Ubeljiji akiitwa Léopold wa Pili (glossing over atrocities committed during the Taifa huru la congo.) Mfalme aliendelea kutoa masharti,
"aliwataka kuto kufanya mabadiliko yoyote mpaka hapo wao watakapo ona kwamba wanaweza kufanya vyema, na kwamba hawakutakiwa kufanya mabadiliko yoyote yaliyo kabidhiwa na kwamba tutaendelea kutoa ushauri".
"Lumumba aliufahamisha umma kwamba uhuru uliotolewa na wabeljiji sio haukuja hivihivi"
" kwa uhuru huu wa Congo hata kama tunasherehekea leo na wabeljiji , nchi rafiki ambayo tupo sawa kwa sawa, hakuna mkongoman hata mmoja ambaye atasahau kwamba vita waliyo yipigana hatimae wakashinda wamaeshinda, kwa mapambano yaliyokuwa yakiendelea,
Mapambano ambayo kwamba watu tulijitoa ambayo kwayo watu walikuwa tayari kwa lolote hata kumwaga damu, kwa namna kwa hakika yalikuwa mapambano matukufu na yalikuwa na mwelekeo wa kukomesha utumwa ambao ulikuwa ukiendeshwa dhidi yetu kwa nguvu"
Hotuba hii ndio ilio kuwa chanzo cha migogoro ya selekari yake pamoja na msimamo wake wa kuitetea nchi yake na kuwataka waberigiji wawaheshimu wakongo na wawaache wajitawale wenyewe bila ya kuingilia katika mambo yao mara kwa mara lumumba alilani mataifa makubwa hasa ya uberigiji, ufaransa na marekani kuchochea vurugu na kupandikiza vikaragosi wao.
[emoji117]KIFO CHAKE [emoji546]
17/1/1961 zilitolewa taalifa kuwa lumumba aliuwawa na masikari alipo kuwa akijalibu kutoroka nchi kwenye mipaka baina ya kongo na Angola.
Lakin zilitoka habari kuwa alikuwa ameshikiliwa na yuko kizuizini lakini mke wake Pauline Lumumba alishuhudia kukamatwa kwa mumewe mjini Ilebo jimboni Kassai-Occidental kabla ya kuuliwa kwake jimboni Katanga Januari 17, 1961.
Barua ya Lumumba kwa Bi-Pauline Aliyoita “risala yangu ya mwisho kwa Pauline” inaaminika na wanahistoria kuwa ni agano kubwa la kisiasa kwa ajili ya vizazi vipya nchini DRC. Kwenye risala hiyo, Emery Patrice Lumumba alisema
"hahofii maisha yake mwenyewe, ikiwa itahitajika kumwaga damu yake ili wakongo wapate uhuru wa kweli, kamwe hawezi kusita."
Emery Patrice Lumumba alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa DRC siku kadhaa kabla ya uhuru wa Kongo Juni 30,1960 kutoka kwa mkoloni wake Ubelgiji.
Hadi sasa mazingira aliyouliwa Patrice Lumumba bado hayajafahamika, lakini utafiti unaelezea kwamba kulikuweko na njama ya nchi za magharibi dhidi ya kiongozi huyo.
Miaka ya hivi karibuni iliyopita bunge la Ubelgiji liliomba serikali yao kukubali kuwa ilihusika kwa fikara na mauwaji ya Lumumba.Vile vile inaelezewa kwamba njama hiyo ilipangwa pia na idara za upelelezi za Marekani na Uingereza, lakini hakuna ushahidi wowote wa madai hayo.
Kwa kumbukumbu ya Lumumba, serikali ya Congo ilitangaza mwaka uliopita kuwa imeunda mji utakaoitwa Lumumbaville. Mji huo unatarajiwa kuweko huko huko Kassai Mashariki ambako alizaliwa Emery Patrice Lumumba.
[emoji117]KIFO CHAKE CHA KUPIGWA RISASI [emoji379]
Lumumba aliuwawa kwa kupigwa risasi na makachero wa kiberigiji na CIA.
Wachambuzi hudai kuwa hotuba yake ndio iliomchimbia kaburi lake.
,"Tumepigana vita hivi vya haki na heshima kumaliza utumwa uliotrushusha hadhi, kulazimisha ukandamizaji wa aibu wa utawala wa kikoloni. Mlitufanyia visa vya kejeli ,matusi na vipigo kila asubuhi, mchana na usikun kwa sababu tu tulikuwa ni weusi. " Mfalme akataka kuondoka mara moja lakini wapambe wakamrai abakie.
Hata hivyo ushindi wa Lumbumba haukudumu muda mrefu, hotuba yake dhidi ya mkoloni mbele ya mfalme ikaiudhi Ubeligiji, ambayo haikutegemea Congo ingejitawala kwa kuwa ikidaidika kutokana na utajiri mkubwac wa mali asili wa taifa hilo.
Waziri mkuu mpya akaandamwa na makundi ya kisiasa nje na ndani. Sehemu ya jeshi iliotumiwa na vibaraka wa Ubeligiji, ikaasi na kutokana na hali hiyo kukazuka uvumi wa visa vya ubakaji dhidi ya wanawake wa Kizungu.
Jeshi la Ubeligiji likapata sababu na kuivamia Congo Julai 10 . siku moja baadae Mkoa wa kusini wa Katanga wenye utajiri wa mkubwa wa maadini yakiwemo ya almasi na shaba ukatangaza kujitenga. Akitengwa na nchi za magharibi na kupewa mgongo na Umoja wa Mataifa, Lumumba akaigeukia Urusi.
Kutokana na hayo ikawa sawa na kusaini adhabu ya kifo chake mwenyewe.
Mpango wa kum,uuwa ukaandaliwa na Shirika la Ujasusi na Marekani na Idara ya usalama ya Ubeligiji, kama serikali ya ubeligiji ilivoykiri binafsi 2002. Patrice lu8mumba aliuwawa Januari 17 ,1961 huko Elizabethville inayojulikana leo kama Katanga.
“Mshirika wake mmoja wa kisiasa wa zamani alimtaja Lumumba kuwa sawa na Nyota iliotanda mbiguni na baadae kutoweka.”Congo imebakia kuwa dola miaka 50 baadae pamoja na misukosuko ilioendelea kuikumba.
Dikteta Mobutu Sese Seko alitawala kwa karibu miaka 40 baada ya kifo cha Lumumba kufuatia mapinduzi yake ya kijeshi hadi 1997.
Mfuasi wa zamani wa Lumumba Laurent desire kabila akamuangusha Mobutu na kutwaa madaraka Januari 2001, miaka 40 baada ya Lumumba.
Vita vya kuwania utajiri wa mali asili ya Congo vinaendelea na katika hili, hata baadhi mataifa ya Umoja wa Ulaya mikono yao pia si safi .
Pamoja na hayo yote, ingawa Lumumba hakuishi muda mrefu baada ya kuikomboa nchi yake, Jina lake bado ni mwenge unaoendelea kuwaka sio tu nchini Congo, bali Afrika kwa jumla.
Makala hii imeletwa kwenu na Dhulkad Madara kutoka morogoro