LEO KATIKA HISTORIA
By Malisa GJ,
Mwaka 1952 Baraza kuu la dola ya Wachagga (Chagga Supreme council) liliketi kumchagua Mangi Mkuu. Wagombea walikua watano. Abdieli Shangali wa Machame, Jackson Kitali wa Mbokomu, Petro Marealle wa Vunjo, John Maruma wa Rombo, na Thomas Marealle wa Marangu.
Baada ya mchujo walibaki Abdiel Shangali (kushoto), Petro Marealle (katikati) na Thomas Marealle (kulia). Baada ya kila mgombea kunadi sera zake, kura zilipigwa na Thomas Marealle kutangazwa mshindi.
Dola ya wachagga ilikua na muundo sawa na dola ya Uingereza (United Kingdoms). Kulikua na "nchi" kadhaa zilizounda dola hiyo. Kwa mfano Old Moshi ilikua na serikali yake, Mangi wake na jeshi lake, vivyo hivyo Uru, Kibosho, Machame, Marangu, Keni etc.
Jumla ya "nchi" 10 zilijiendesha independently, kisha zikaunda serikali ya pamoja (Federal government). Mangi Mkuu ndiye aliyekuwa Kiongozi mkuu wa "Federal government" iliyounganisha "nchi" zote 10. Alichaguliwa na Baraza la kuu la uongozi (Supreme council) ambacho kilikua chombo kikuu cha kusimamia utendaji wa serikali. Kiliundwa na Wamangi na Wachili.
Federal government ilisimamia mambo ya pamoja kama vile uchumi, diplomasia na mambo ya nje, huku mambo mengine kama miundombinu, elimu na afya yakiachwa kwa serikali za "nchi" husika.
Federal government ilifanikiwa kuanzisha sarafu yake, kuunda bendera ya shirikisho na kufungua ofisi za ubalozi Uingereza, Zanzibar na Oman. Pia mwaka 1920 ilianzisha gazeti lake lililoitwa KOMKYA, ambalo lilikua gazeti la kwanza la wazawa Afrika mashariki kabla ya Buruuli la Buganda na Imperial la Zanzibar yaliyoanzishwa 1930.
Moja ya sababu iliyomfanya Thomas Marealle kushinda kiti cha Umangi Mkuu ni elimu. Alikua mgombea pekee mwenye shahada ya uzamili (masters degree) wakati huo.
Wakati Tanganyika inapata Uhuru kulikua wachumi wawili tu wazawa ambao ni Thomas Marealle na Fredrick Mchauru. Wote wawili walisoma London School of Economics na kutunukiwa shahada za uchumi. Lakini Marealle alipata ufadhili kwenda Cambridge University (Trinity College) kufanya shahada ya pili ya uchumi.
NB: Picha ya pili, Mangi Marealle akihutubia "Chagga Supreme Council" mara baada ya kutangazwa mshindi.!