Katika maendeleo ya mtu mmoja mmoja yaani per capita development mpo nyuma sana na hata Kenya tupo nyuma. Mkenya mmoja au Mtanzania mmoja ni masikini kushinda Mshelisheli mmoja. Maana serikali ya ushelisheli ina eneo ndogo sana ya kujenga miundombinu na watu wachache wa kulisha na kusomesha. Ila pia kuna nchi ndogo mbovu tu kama Burundi ambayo ina watu wachache na ardhi ndogo ila Mburundi mmoja ni masikini kushinda Mtanzania mmoja. Yaani wale wamezembea kinyama hata kuwashinda licha ya nyinyi kuwa na watu wengi wa kulisha na kusomesha na kufungia maji na kufungia umeme. Kiuchumi tunasema Burundi has smaller Gni per capita than Tanzania na ndio maana Burundi bado ni Ldc na TZ ni middle income. Yaani ni aibu kubwa sana nchi ndogo kushindwa kulisha watu wake au kuwajengea barabara. Burundi ni kama nyumba ya watoto watatu ilhali wazazi wao wameshindwa kuwalisha au kuwasomesha na Tanzania ni kama nyumba ya watoto kumi na watano ilhali wazazi wamejitahidi na kulisha watoto wote na kusomesha watoto wote hadi angalau wakamaliza shule ya msingi, japo hawana uwezo wa kuendelea na masomo zaidi. Nadhani utakuwa umenielewa.