"Africa-Korea Summit" Korea Kusini Yasaini Mikataba 50 na Nchi za Afrika, Yaahidi Kutoa Misaada ya Dola Bilioni 10

"Africa-Korea Summit" Korea Kusini Yasaini Mikataba 50 na Nchi za Afrika, Yaahidi Kutoa Misaada ya Dola Bilioni 10

Kale kanchi kalivyo kadogo kanaikopesha Africa nzima,

Something is wrong with the way we run our economies
Ni vigumu sana kumeza ukweli mchungu. South Korea ilikuwa maskini sana na mwaka 1964 walikumbwa na njaa kali sana iliyotokana na mavuno hafifu ya mpunga waliyokuwa wamepata mwaka 1963 na ilipofika mwezi wa nne 1964 wakawa hawana akiba ya chakula kabisa. Walipata misaada kutoka nchi za nje ambapo serikali ya Tanganyika iliwapa msaada wa $1000.

Baada ya Nyerere kuanzisha "Vijiji vya Ujamaa" mwaka 1967, rais wa South Korea bwana Park Chung-hee aliipenda sera hiyo ya Nyerere ya kuhimiza maendeleo vijijini, kwa hiyo na yeye mwaka 1970 akaanzisha kile alichoita "Saemaul Undong" kwa maana ya "Jumuia Mpya ya Vijijini". Leo hii, "Vijiji vya Ujamaa" Tanzania vimekuwa kama jehanamu wakati "Saemaul Undong" za South Korea zote zimegeuka kuwa majiji makubwa yenye viwanda vizito.
 
Unaweza weka economic statistics za Korea vs Tanzania ,katika miaka hiyo ya 60 hadi 70...!?
 
Korea Kusini imesaini mikataba 50 ya biashara,mikopo na sekta za Rasilimali na Nchi za Afrika ikiwemo Tanzania.

Rais wa Korea amesema anaendesha sera ya ushirikiano wenye faida kwa.pande Mbili huku akisema Nchi yake itaongeza Msaada Kwa Nchi za Afrika Hadi Dola Bilioni 10 ndani ya miaka 5 ijayo.

Aidha amesema atapanua biashara baina ya Afrika na Korea Hadi kufikia Dola Bilioni 14.
---
Takriban makubaliano na mikataba 50 imetiwa saini wakati wa mkutano wa kwanza wa kilele wa Korea Kusini na viongozi kutoka nchi 48 za Afrika, ili kushirikiana katika masuala yanayohusu madini, nishati na utengenezaji wa bidhaa, wizara ya viwanda ya Korea Kusini ilisema Jumatano.

Kampuni ya Korea Kusini ya Hyosung Corp ilitia saini mkataba wa kusambaza transfoma za umeme nchini Msumbiji zenye thamani ya dola milioni 30, wizara ilisema katika taarifa.

Wizara ya viwanda pia ilitia saini makubaliano ya kushirikiana katika madini muhimu na Madagaska na Tanzania, ili kupata vifaa kwa ajili ya viwanda kama vile betri, ilisema taarifa hiyo.

Makubaliano hayo 47 na mataifa 23 ya Afrika yalifanywa wakati wa mkutano huo huku nchi hiyo ya nne kwa ukubwa wa kiuchumi barani Asia, ikinuia kupata soko kubwa la nje, barani Afrika.

"Pamoja na uwezo wake mkubwa, Afrika bado inachangia asilimia 1-2 tu ya biashara na uwekezaji wa Korea Kusini..." Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol aliuambia mkutano huo wa kibiashara, wa viongozi 200 wa kisiasa na viwanda kutoka nchi za Afrika na Korea Kusini, siku ya Jumatano.

"Matumaini yangu ni kwamba ushirikiano wa rasilimali wenye manufaa kwa pande zote utapanuliwa," Yoon alisema.

Yoon aliahidi Jumanne kwamba Korea Kusini itaongeza msaada wa maendeleo kwa Afrika hadi dola bilioni 10 katika kipindi cha miaka sita ijayo, na kusema itatoa dola bilioni 14 katika ufadhili wa mauzo ya nje ili kukuza biashara na uwekezaji kwa makampuni ya Korea Kusini barani Afrika.

VOA.

My Take
South-South Cooperation ni Muhimu zaidi kiuchumi kuliko Ushirika na West,Russia na China.
---

South Korea agrees to lend billions to Tanzania, Ethiopia​

Tanzania and Ethiopia said they had signed accords with South Korea for loans of billions of dollars, part of broader deals that will give the Asian nation access to Africa's crucial mineral resources and vast export market.

South Korea is hosting at least 30 heads of state, including Tanzania and Ethiopia, at a South Korea-Africa summit this week.

Tanzania said it will borrow $2.5 billion over the next five years from South Korea through concessional loans.

The country also signed two accords on Korean use of its ocean resources and minerals used in clean energy technologies such as nickel, lithium and graphite, presidential spokesperson Zuhura Yunus said on Sunday.

Ethiopia, a fast-growing economy with 126 million people, signed a $1 billion financing deal over four years for infrastructure, science and technology, health and urban development, the state-affiliated Fana media outlet said.

Tanzanian President Samia Suluhu Hassan is also seeking cooperation in sectors including sustainable use of ocean resources, development of natural gas deposits and creative industries, and for Tanzania to supply labour to South Korea, according to Yunus.

Since Friday, South Korean President Yoon Suk Yeol has held meetings with the leaders of Sierra Leone, Tanzania and Ethiopia and was due to meet separately with heads of other states including Zimbabwe, Togo, Rwanda and Mozambique on Monday.

View: https://twitter.com/VOASwahili/status/1798470400625746431?t=QGuPmDD1b-XBp-VGpm7O2A&s=19
 
Ni aibu nchi 18 zimejaa madini, mito, mbuga, maziwa, bahari, misitu, idadi ya watu kuzidiwa akili na Korea kusini nchi moja
 
Kina samia na ruto pamoja na wenzao wengine walioenda huko korea wanaona poa tu kupewa misaada na mikopo na ka nchi kadogo. Ila ni aibu kubwa afrika kusaidiwa na ka nchi wakati afrika ni giant ina rasimali za nyingi za kutosha kujiletea maendeleo yenyewe. Inasikitisha kwa kweli
Mbaya zaidi haya hata aibu asee, yote yameenda kupanga msitari kuomba ni aibu kubwa sn
 
Huu umasikini wa afrika ni aibu kwa kweli. Masikini wameenda kujazana nyumbani kwa tajiri wasaidiwe, kila masikini kapewa msaada wake. Tajiri anajua katoa jumla ni kiasi gani amesaidia. Ipo siku naye atakuja nyumbani kwa masikini apatiwe anachokihitaji. Haijulikani ni karne ya ngapi afrika itaacha kuombaomba misaada kwa matajiri
 
Unaenda kuomba kwenye nchi ndogo kama ile ma-Rais 18 hamuoni hata aibu
ruto akihojiwa na bbc anadadavua na kufaragua misaada ya mikopo ya korea kwa afrika bila aibu. Inatakiwa atokee kiongozi muafrika aone aibu kukimbilia kuombaomba huko nje. Nchi za afrika zijitosheleze zenyewe kwa rasilimali zao. Kama ni biashara ni nipe nikupe, leta hela upate malighafi na sio kwenda kuombaomba mwisho wa nchi ni kuishia kwenye masharti magumu ya kuja kunyonywa rasirimali za nchi
 
ruto akihojiwa na bbc anadadavua na kufaragua misaada ya mikopo ya korea kwa afrika bila aibu. Inatakiwa atokee kiongozi muafrika aone aibu kukimbilia kuombaomba huko nje. Nchi za afrika zijitosheleze zenyewe kwa rasilimali zao. Kama ni biashara ni nipe nikupe, leta hela upate malighafi na sio kwenda kuombaomba mwisho wa nchi ni kuishia kwenye masharti magumu ya kuja kunyonywa rasirimali za nchi
Ni mambo ya kijinga haswa
 
Ilitakiwa sisi waafrika ndio tupeleke watu wetu wakafundishwe kutengeneza uchumi, wakasome huko tunakoomba misaada, wakirudi nyumbani nasi tunakuwa na viwanda vya kutengeneza zana mbalimbali za kujenga barabara, kuchimba madini, kutengeneza vyombo vya elekroniniki na mashine zingine. Misaada ya kupewa akili za kujikwamua sisi wenyewe ni si kupewa hela. Tuna vitu vya kutupatia hela hatuhitaji mikopo
 
Back
Top Bottom