"Africa-Korea Summit" Korea Kusini Yasaini Mikataba 50 na Nchi za Afrika, Yaahidi Kutoa Misaada ya Dola Bilioni 10

Kale kanchi kalivyo kadogo kanaikopesha Africa nzima,

Something is wrong with the way we run our economies
Ni vigumu sana kumeza ukweli mchungu. South Korea ilikuwa maskini sana na mwaka 1964 walikumbwa na njaa kali sana iliyotokana na mavuno hafifu ya mpunga waliyokuwa wamepata mwaka 1963 na ilipofika mwezi wa nne 1964 wakawa hawana akiba ya chakula kabisa. Walipata misaada kutoka nchi za nje ambapo serikali ya Tanganyika iliwapa msaada wa $1000.

Baada ya Nyerere kuanzisha "Vijiji vya Ujamaa" mwaka 1967, rais wa South Korea bwana Park Chung-hee aliipenda sera hiyo ya Nyerere ya kuhimiza maendeleo vijijini, kwa hiyo na yeye mwaka 1970 akaanzisha kile alichoita "Saemaul Undong" kwa maana ya "Jumuia Mpya ya Vijijini". Leo hii, "Vijiji vya Ujamaa" Tanzania vimekuwa kama jehanamu wakati "Saemaul Undong" za South Korea zote zimegeuka kuwa majiji makubwa yenye viwanda vizito.
 
Unaweza weka economic statistics za Korea vs Tanzania ,katika miaka hiyo ya 60 hadi 70...!?
 

View: https://twitter.com/VOASwahili/status/1798470400625746431?t=QGuPmDD1b-XBp-VGpm7O2A&s=19
 
Ni aibu nchi 18 zimejaa madini, mito, mbuga, maziwa, bahari, misitu, idadi ya watu kuzidiwa akili na Korea kusini nchi moja
 
Mbaya zaidi haya hata aibu asee, yote yameenda kupanga msitari kuomba ni aibu kubwa sn
 
Huu umasikini wa afrika ni aibu kwa kweli. Masikini wameenda kujazana nyumbani kwa tajiri wasaidiwe, kila masikini kapewa msaada wake. Tajiri anajua katoa jumla ni kiasi gani amesaidia. Ipo siku naye atakuja nyumbani kwa masikini apatiwe anachokihitaji. Haijulikani ni karne ya ngapi afrika itaacha kuombaomba misaada kwa matajiri
 
Unaenda kuomba kwenye nchi ndogo kama ile ma-Rais 18 hamuoni hata aibu
ruto akihojiwa na bbc anadadavua na kufaragua misaada ya mikopo ya korea kwa afrika bila aibu. Inatakiwa atokee kiongozi muafrika aone aibu kukimbilia kuombaomba huko nje. Nchi za afrika zijitosheleze zenyewe kwa rasilimali zao. Kama ni biashara ni nipe nikupe, leta hela upate malighafi na sio kwenda kuombaomba mwisho wa nchi ni kuishia kwenye masharti magumu ya kuja kunyonywa rasirimali za nchi
 
Ni mambo ya kijinga haswa
 
Ilitakiwa sisi waafrika ndio tupeleke watu wetu wakafundishwe kutengeneza uchumi, wakasome huko tunakoomba misaada, wakirudi nyumbani nasi tunakuwa na viwanda vya kutengeneza zana mbalimbali za kujenga barabara, kuchimba madini, kutengeneza vyombo vya elekroniniki na mashine zingine. Misaada ya kupewa akili za kujikwamua sisi wenyewe ni si kupewa hela. Tuna vitu vya kutupatia hela hatuhitaji mikopo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…