Africa Kusini nchi ngumu

Africa Kusini nchi ngumu

Forfofo

Senior Member
Joined
Aug 22, 2024
Posts
161
Reaction score
359
Umefika hatua hata ukitaka kumsaidia mtu anakuhisi unataka kumtapeli.

Kwa madiba palinishangaza sana, watu wanaishi kwa kuliana Timing, hii inasababisha hata ukitaka kumsaidia mtu anahisi unataka kumtapeli.

Ilikuwa siku moja nipo Johannesburg katika mji wa Germiston, nikamsikia jamaa mmoja anaongea kiswahili fulan japo ilikuwa na lafudhi ya Kenya hivi nikasema mwenzangu huyu hata tupige stori moja mbili tatu za hapa(japo kuwa mimi nilikuwa napita naenda nchi nyingine).

Nilishangaa sana jamaa kaniruka tena kwa maneno ya kunishangaza, mwenyeji wangu nilipomsimulia hii kisa akanambia S. Afrika usimuamini mtu hiyo ni kanuni yakwanza ambayo ni lazima uifate. Kwangu mimi niliona km ni kanuni inayoweza kukunyima fursa mpya maana kuna mwingine atataka akusaidie tuu.
 
Wabongo ukiacha ujinga mwingi tulionao, tuna ujamaa sana. Tunapenda kuchangamana. Hata mimi nikiwa nje huko nikasikia mbongo ama mtu anaongea kiswahili lazima nitake kumpa salamu kidogo.

Hata hapa bongo nikikutana na mtu ama nikamsikia anaongea lugha ya nyumbani kwetu lazima nitake kumsalimia tuongee kidogo kikwetu. Sema niliwahi kukutana na mshikaji nimesoma nae Primary tunapiga kilugja fresh, nikamsemesha kilugha hapa Dar akasema hakijui nilichoka sana.
 
Ni kupotezeana muda unaweza kuta mtu amekukuta kwenye dimbwi la fikra na halmashauri ya ubongo wako kisha anakuletea Stori za kipuuzi.
Hapana kaka, watu wanashida south, unaweza ukawa na uwezo wa kumsaidia hata kwa ushauri au kumuunganishia kazi lkn wao uhisi unamtapeli
 
Back
Top Bottom