tuusan natumai kwamba sasa utaelewa point yangu kwamba Kenya watu wengi wanamiliki magari kushinda Tanzania kwa hivyo expressway itapata wateja na wala sio kwamba wanafinywa maana wanalipa toll kwa hiari yao. Yaani
tuusan hio statistic hapo juu maana yake ni hivi maana huwa napenda kubreak down vitu into simple language ili hata mama mboga aelewe:
Ukichukua watu elfu moja Tanzania randomly (wengine kutoka Dar, wengine Kigoma, wengine Tanga e.t.c) kisha ukawaambia wanaomiliki gari wainue mkono juu basi kati ya hao watu elfu moja ni watu saba tu watakaoinua mkono. Yaani kwa kila Watanzania elfu moja wasaba tu ndio wanamiliki gari.
Tukija upande wa Kenya, ukichukua Wakenya elfu moja randomly (wengine kutoka Nairobi, wengine Turkana, wengine Mandera, wengine Mombasa) na kuwaambia kwamba wanaomiliki gari wainue mkono juu basi kati ya hao Wakenya elfu moja Wakenya sabini watainua mkono juu. Yaani nikisema kwamba Mkenya mmoja mmoja ana pesa kushinda Mtanzania mmoja mmoja huwa mnaona kama ni utani. Hata kwenye kumiliki TV au Laptop nipo sure Mkenya mmoja mmoja anamiliki TV au Laptop kwa wingi kushinda Mtanzania mmoja mmoja. Hata umiliki wa baiskeli au pikipiki ni vivyo hivyo tu. Hata umiliki wa helicopter ni vivyo hivyo maana wakati wa Siasa Uganda na Tanzania huwa mnakuja Kenya kuagiza helicopter za wanasiasa wetu ili mkapige campaign nazo. Nyinyi mnatushinda tu kwa mlo. Yaani Mtanzania mmoja mmoja anashiba kushinda Mkenya mmoja mmoja, hii ni kwa sababu nchi yenu inapokea mvua kwenye 100% ya ardhi yenu ilhali Kenya 75% ya ardhi ni arid or semi-arid.
Cc
Geza Ulole joto la jiwe ichoboy01 Shebby01 The best 007
Uhuru n Umoja