African Sports, Mwadui kucheza fainali Jumapili

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,319
​

Timu za African Sports ya Tanga na Mwadui FC ya Shinyanga zinatrajiwa kucheza mchezo wa fainali ya kusaka Bingwa wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) siku ya jumapili katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.


African Sports waliibuka washindi wa kwanza. katika Kundi A, na Mwadui FC washindi wa kwanza Kundi B watacheza mchezo huo wa fainali ambapo Bingwa atapewa zawadi ya Kombe na medali, hali kadhalika kwa msindi wa pili.

Chanzo: African Sports
 
Mwadui inabidi afate nyayo za watoto wa mjini Stand UTD Chama la Wana!! si tulibeba ndoo na bungeni tukaenda v
 
Mwaduni wapo vizuri sana kwa sasa bila shaka watashinda
Kocha Jamhuri Kiwero
 
Irushwe basi na azamtv ili tuone huo mpambano wa kukatana shoka
 
Japo msimu uliopita kulikua na fitina fitina ila kwa hili la kuifanya ligi dalaja la kwanza angalau wadau wanaifatiria Jamal Malinzi anaitaji sifa.

Kilicho baki ni kutafuta wadhamini na pia kuwa thamini wachezaji wa uko ili tupate timu ya taifa oliyobora sio bora timu.!

TFF wajitahidi waanzishe ligi ya tff itakayo jumuisha vilabu vyote vilivyosajiliwa Tanzania na Zanzibar hii itasaidia wachezaji kucheza mechi nyingi.
 
Mkuu Ndetichia yaani huu mpambano ni wa kukatana shoka, ilipaswa uoneshwe ili tuaone hawa wachimba madini wa kule Shinyanga dhidi ya Africans sports.
 
mwadui fc tayari ni bingwa

Na-declare intetest: Mwadui FC ni timu ya nyumbani kabisaaa!

Pamoja na hayo, siipendi kwa sababu ya Julio. Amejitapa atachukua kombe la ligi kuu msimu ujao, akichemka atakuwa wa pili akichemka sana nafasi ya tatu ni yake (RFA michezo, 16/02/2015). Julio akifukuzwa nitarejesha mapenzi kwa Mwadui FC, kwa sasa naiombea African Sports iichakaze vilivyo timu ya nyumbani, Mwadui FC ili Julio atulie!
 
Stand Utd haishuki, mwaka kesho Inshaallah, jiandae kushuhudia Shinyanga Derby.

Kama stand united haitashuka daraja basi ligi kuu mwakani itakuwa na DERBY nne, Itakuwepo ile ya COAST UNION VS AFRICAN SPORTS kule Tanga, MBEYA CITY VS PRISON kule Mbeya, YANGA VS SIMBA Dar es salaam, na nyingine ni ile ya STAND UNITED VS MWADUI FC huko Shinyanga.
 
Viva la toto afrka,African sports
 
Mtaji wa yanga huo. Yanga jiandaeni kupata point kumi nambili hizoo.
 

Derby maanake nn? Hizi sio derby?
1. MTIBWA v POLISI MORO
2. AZAM v SIMBA
3. AZAM v YANGA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…