friendfx
JF-Expert Member
- Oct 16, 2017
- 247
- 256
Libya ya hayati Gadaffi inanuka damu. Nchi ya Mali neno 'Amani' ni msamiati adimu ambao haupatikani kwenye kitabu chochote kilicho ndani ya taifa lao. Congo DRC mvua ya vita inanyesha through out the year. Sudan kusini kumetulia kidogo kwa sasa.
Lakini kama ukisikia kesho vita vimeanza, naomba usione kama ni habari inayostahili kupewa heading ya "Breaking news."
Vita inapiganwa Tripoli, vikao vya usuluhishi wanaviongoza wazungu Moscow Urusi. Umoja wa nchi huru za Africa upo hai kwenye maandishi ya vitabu vilivyo pale Adis Ababa Ethipio. Ila ki uhalisia (AU ) ni kama maiti iliyotolewa mochwari ikisubiri kusomewa ibada ya maziko."
Wakoloni waliozipatia Uhuru nchi za Afrika walitengeneza mfumo wa siri. Mfumo ambao Africa itaendelea kuwa tegemezi kwao kwa zaidi ya miaka 100.
Kulielewa andiko hili lazima uwe timamu kifikra, ndipo tutasafiri pamoja kwenye hii safari yenye hisia za kuumiza.
Leo ni miaka 50+ tangu nchi za Africa zipate uhuru. Lakini nch nyingi bado zinahangaika kujenga miundo mbinu ya barabara za mijini. Wao wazungu wanahangaika kufanya tafiti ili siku moja wayahamishie maisha sayari ya Mars.
Kwanini Africa ndilo bara lililobeba idadi kubwa ya maskini duniani? Ni sababu ya kuwa na watu wengi ambao hawana uhakika wa kula. Na katika viwango vya umaskini, umaskini wa kiwango cha mwisho kabisa duniani. Ni ule wa mtu kutokuwa na uhakika wa kula chochote inapofika kesho. Aina hii ya umaskini ndio inayolila bara la Africa.
"Robert Mugabe" alijaribu kuleta jeuri ya kuonyesha hatishwi wala hababaishwi na wazungu. Akataka kuionyesha dunia kwa vitendo, "Zimbabwe" litakuwa ni taifa la kwanza ndani ya Africa kujiendesha bila sapoti ya wazungu. Akanyang'anya mashamba yao akagawa kwa maskini wa Zimbabwe.
Kila alipopata fursa ya kuzikanyaga sakafu za umoja wa mataifa. Mugabe alikuwa anaziogesha mate ya ghadhabu microphone za UN. Kinywa chake kilikuwa kiki washambulia mabeberu kwa hotuba zenye maneno makali, yenye hisia za kejeli na maudhi.
Lakini mission yake haikufanikiwa, sababu wazungu walipokabidhi Uhuru kwa nchi za Africa. Kuna siri nzito waliificha ndani ya vitabu vyao. Na hili Africa itoke kwenye mkwamo huu ni lazima watawala wafunguliwe milango ya fikra, na sio milango ya V8.
Mugabe aliamini anaweza kuimarisha uchumi wa Zimbambwe bila msaada wa pesa ya mabeberu.
Lakini mpaka mauti inamuingiza ndani ya kaburi. Macho yake hayakuwahi kushuhudia anachokifikiri. Zaidi akaiacha Zimbabwe ikiwa kwenye jalala la ufukara, ikinuka uvundo wa dhiki na marashi ya umaskini. Pesa ikawa inashuka thamani kwa kasi ya kutisha.
Mugabe hakujua tiba gani aitumie kuimarisha afya ya uchumi wa Zimbambwe. Akaamua kuipungia mkono wa buriani dunia. Akiwa na ubongo uliobeba ndoto aliyoshindwa kuigeuza kuwa simulizi ya kweli."
, tamanio la kiongozi wetu la kuona siku moja nchi za Africa ziki zi saidia nchi za kizungu kiuchumi. Hili ni wazo jema lenye afya, na tamanio la mwa Africa yoyote timamu anayechukia utegemezi. Sababu hata Mwalimu Nyerere aliwahi kusema wazi.
"NCHI MASKINI HAIWEZI KUJITAWALA KAMA INATEGEMEA MSAADA KUTOKA NCHI ZA NJE."
Hata mimi naamini, kuna siku Africa itakuja kuwasaidia wazungu, sababu Africa ina kila rasilimali. Lakini siku hiyo ikifika wazungu wao tayari watakuwa wanaishi sayari ya Mars."