Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Shirika la Afya Duniani (WHO) inakadiria kuwa watu 100000 wa Afrika hufa kwa dawa bandia. Ilikadiriwa kuwa mwaka 2015 watoto 122,000 chini ya miaka mitano walifariki kwa kutumia dawa zisizo na ubora za kuzuia malaria kusini mwa jangwa la Sahara
Utawala dhaifu, huduma mbovu za afya na wimbi la umasikini umesababisha kukua kwa hili soko la dawa zisizo na ubora, na dawa bandia
Tangu mwaka 2013, Afrika imechukua takribani asilimia 42 ya dawa feki duniani
Wataalamu wanasema dawa hizo mara nyingi huwa zimeisha muda wake wa matumizi au ziko chini ya kiwango, au dawa za kughushi (Counterfeit)
Ni vigumu kuwajua watengenezaji
Katika harakati za kukabiliana na janga hilo, marais kutoka nchi saba - Jamhuri ya Kongo, Gambia, Ghana, Niger, Senegal, Togo na Uganda - wanakutana Ijumaa huko Lome kusaini makubaliano ya uhalifu wa usafirishaji wa madawa feki
Kusudi ni kukuza ushirikiano kati ya serikali na kuhamasisha mataifa mengine ya Afrika kujiunga na mpango huu.
Lakini hata viongozi wanatambua, jukumu la kumaliza utitiri wa dawa bandia ni mkubwa
"Ni ngumu sana kufuatilia ni wapi dawa bandia zinatoka," Dk. Innocent Kounde Kpeto, rais wa chama cha wafamasia wa Togo
"Nchi ambazo zinatajwa mara nyingi sio nchi za asili za utengenezaji wa dawa hizi. Watengenezaji huficha maeneo yao ili wasitambulike".
Kpeto alisema Inakadiriwa kuwa kati ya asilimia 30 hadi 60 ya dawa inayouzwa barani Afrika ni bandia na mengi yanatoka China na India
Jaribio la kukwepa mafuriko mabaya ya bidhaa bandia yanaendelea vizuri
Baadhi ya sehemu zilizosadikiwa kuwa chanzo cha dawa hizo zimebomolewa, kama vile soko la Adjegounle huko Cotonou ambalo lilifanya kama lango kuu la dawa feki kuelekea Nigeria.
Novemba mwaka jana, polisi huko Ivory Coast walikamata tani 200 huko Abidjan na kuwakamata watuhumiwa wanne akiwemo raia wa China
Togo ni moja wapo ya nchi za waasisi katika kuzuia mtiririko wa dawa bandia
Ilibadilisha sheria mnamo mwaka wa 2015 na sasa wafanyabiashara wanaoweza kwenda jela miaka 20 na kulipa faini ya dola 85,000 (euro 75,000)
Chanzo: Daily Monitor