Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 20,654
- 35,887
Afrika ya zama za Mwl Nyerere, Nkrumah, Jomo Kenyatta, Mobutu Seseseko, Augustino Neto. Tulishuhudia mapinduzi kila uchao sababu kubwa ilikuwa pengine uchanga wa nchi husika, maslahi ya wakoloni, upendeleo katika ugawaji wa rasilimali na nk.
Kidogo Afrika ilipumzika katika zama za mapinduzi ya kijeshi, nchi kama Nigeria, Mali na Uganda zilitia aibu na doa kubwa katika bara letu na kuonekana kama bado tuka katika zama za mawe.
Hivi karibuni hali ya mapinduzi imerejea kwa kasi kubwa sijui kwanini nchi za Kaskazini zimekuwa zikinyemelewa na mapinduzi ya mara kwa mara.