Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,657
- 20,967
Habarini wakuu.
Iko hivi, utafiti wa dawa hadi ikaingia sokoni ni gharama kubwa sana na una mlolongo mrefu balaa.
Hugharimu mabilioni ya dola na makumi ya miaka.
Makampuni mengi kabla ya kufanya utafiti wa dawa kwanza huangalia kama italipa? Je wanaoumwa wanaweza kununua dawa? Hii imepelekea makampuni kuacha kufanya utafiti kwaajili ya magonjwa ya kimaskini. Leo huwezi kuta kampuni kubwa liko serious na chanjo ya malaria au magonjwa ya kuhara.
Umeona leo ugonjwa wa Corona uliowaathiri sana wenye hela ulivyopiganwa, kila kona wanagundua kinga .
Ingefaa waafrika, au nchi za Africa tuchangishane pesa za kujenga na kuendesha taasisi ya kutafiti chanjo na tiba ya magonjwa yanayotusumbua.
Tupate chanjo ya UKIMWI, Malaria nk.