Afrika Inazama

Afrika Inazama

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,048
Reaction score
22,790
1651959809301.png

Afrika inazama.

Tujiiulize: Tunazama kwenye nini? Umaskini? Madeni? Ujinga? Magonjwa? Dhuluma? .....

Nini la kufanya ili tusiendelee kuzama?
 
View attachment 2215995
Afrika inazama.

Tujiiulize: Tunazama kwenye nini? Umaskini? Madeni? Ujinga? Magonjwa? Dhuluma? .....

Nini la kufanya ili tusiendelee kuzama?
Tunazama kwenye ujinga na kufuata dini/imani za kuletewa ili tutawalike vizuri zaidi tukiamini vya kuletewa na wenzetu ndiyo mali zaidi. Tukiendelea kupeleka watoto wetu na kuwaaminisha kuwa madrasat ni bora kuliko elimu basi tumekwisha.
 
Jahazi linapozama abiria huamua ili waweze kuwa hai kipi wakitose baharini kwanza na endapo litaendelea kuzama watachagua hivyohivyo mpaka kufikia wagonjwa na wadhaifu wakiwamo wazee na watoto.
Afrika viongozi waliopigania uhuru licha ya kuwa wasomi bora kuliko hawa walikufa masikini na hawa wa sasa ni matajiri kuliko wafanyabiashara huku hawalipi kodi!
Kheri wabaki watu wachache watakao liendeleza bara hili kuliko kuwa na utitiri ambao watalizamisha jahazi(bara).
 
Mbona siku zote tumo shimoni...tuzame mara ngapi?
Tulikuwa tunatapatapa kwenye maji ya kina kifupi tukidhani tutajikwamua, sasa hivi tunazama kwenye maji ya kina krefu.
 
Jahazi linapozama abiria huamua ili waweze kuwa hai kipi wakitose baharini kwanza na endapo litaendelea kuzama watachagua hivyohivyo mpaka kufikia wagonjwa na wadhaifu wakiwamo wazee na watoto.
Afrika viongozi waliopigania uhuru licha ya kuwa wasomi bora kuliko hawa walikufa masikini na hawa wa sasa ni matajiri kuliko wafanyabiashara huku hawalipi kodi!
Kheri wabaki watu wachache watakao liendeleza bara hili kuliko kuwa na utitiri ambao watalizamisha jahazi(bara).
Walipigania UHURU wa maisha yao na sio wa waafrika wote zaidi ya kuwahadaa.Hao waliopigania UHURU ndio walioweka misingi mibovu hata hawa waliopo sasa wamepikwa nao hao waliofariki.Hakuna mpigania UHURU aliyekufa masikini mbona wameacha uzao wao wakiwa matajiri.
 
Wapigania UHURU walihadaa waafrika wakawafukuza wakoloni kisha wao wakawa wakoloni weusi, wakijilimisha utajiri wa nchi wao na vizazi vyao huku mamilioni ya waafrika wakitopea kwenye ufukara zaidi ya wakati wa mkoloni. Viwanda, mashamba, na miradi yote waliyoacha wakoloni imekufa. Huku familia za wapigania UHURU wakiwa mamilionea wakiishi kifahari.Bora mkoloni mweupe kuliko mkoloni mweusi,kwani maisha yalikuwa bora ajira tele mashambani, viwanda, elimu, afya miundombinu zilikuwa bora kabisa, huku wakulima wakiwa na uhakika kabisa pa kuuzia mazo yao bila shida kabisa.
Afrika inazama. Mugabe, kamuzu banda, savimbi ni waafrika tena wasomi wa juu walizitumia elimu zao kuzibomoa nchi zao.
 
Kitu Gani kimeashiria hivyo?
Maendelo ya Bara la afrika ukilingansiha na mabara mengine yaliyokuwa kiwango kimoja mwaka 1960. Leo hii tunaomba misaada kutoka China ambayo ilikuwa maskini kuliko sisi miaka hiyo. Najua unaweza kusema "walitujengea reli ya Uhuru na kiwanda cha Urafiki", lakini hujui yaliyokuwapo nyuma ya misaada hiyo, jambo ambalo ni mjadala mwingine.
 
Tukiacha kulinganisha...Africa ya miaka ya 60 Na ya Sasa Ni ipi Ina afadhali?
 
Tukiacha kulinganisha...Africa ya miaka ya 60 Na ya Sasa Ni ipi Ina afadhali?
Maisha ni one way traffic, huwezi kusema mtu fulani ana afadhali leo kwani alikuwa na hali mbaya utotoni, na ukashindwa kulinganisha hali yake leo na wale aliozaliwa nao kipindi kimoja. Opportunities zilizokuwapo zamani ni tofauti na zilizopo leo
 
Back
Top Bottom