Afrika kazi bado ipo, nimeshangaa kwamba Tanzania bado ni koloni la Ujerumani

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Nimekutana na taarifa kwamba bunge la Ujerumani limekaa vikao kujadili mradi wa umeme wa Stiegler George kule Tanzania, na wakapiga kura ya kuupiga chini huo mradi. Hizi taarifa nimeshindwa kuzimeza maana zimenipa hasira, utani wa jadi pembeni, yaani wazungu wakalie vikao mradi ambao haupo hata kwenye bara lao huko Ulaya, kha Afrika kweli tuna shughuli, tena ndefu.

Maskini Watanzania, haya mjiandae kupokea amri kutoka kwa bwana mkuu, maana Mjerumani bado anawamiliki hata baada ya kusemekana kaachia enzi za ukoloni.
--------------------------------------

Ujerumani: Mradi wa umeme wa Tanzania wapigiwa kura bungeni
Bunge la Ujerumani limepitisha mswada wa kuitaka serikali ya Ujerumani itafute njia mbadala ya mradi wa Tanzania wa kuzalisha nishati ya umeme kwenye bonde la Stiegler ili kulinda turathi na asili.

Vyama vilivyomo katika serikali ya mseto ya Ujerumani vimeitaka serikali itafute njia nyingine badala ya ile ya mradi wa kuzalisha nishati ya umeme kwenye bonde la Stiegler kwenye mto rufiji kusini mwa Tanzania Wabunge wa vyama vya CDU/CSU, Kijani na AFD walishiriki katika kupiga kura hiyo lakini chama cha mrengo mkali wa kulia cha AfD, hakikushiriki. Azimio la vyama vya CDU,CSU na SPD pia linatokana na mapendekezo ya kamati ya serikali ya Ujerumani ya ushirikiano wa kiuchumi.
Azimio lililopitishwa bungeni na vyama hiyvo vilivyomo katika serikali ya mseto ya Ujerumani linaitaka serikali kuu isaidie katika masuluhisho ya kukidhi mahitaji ya nishati ya Tanzania bila ya kuathiri mazingira. Katika azimio lao vyama hivyo vimesema mradi huo mkubwa wa kuzalisha nishati ya umeme utavuruga mfumo wa mto mmojawapo mkubwa barani Afrika.

Tanzania inakusudia kujenga bwawa kubwa la kuzalisha nishati ya umeme kwa kutumia nguvu ya maji kutoka kwenye mto rufiji. Sehemu hiyo ni muhimu kwa shughuli za kilimo za wakaazi. Ikiwa mradi huo utaendelea mbele bonde la Stiegler ambalo limewekwa miongoni mwa turathi za shirika la Umoja wa mataifa la UNESCO litapoteza hadhi yake na huenda likasababisha athari kubwa katika raslimali zilizopo kwenye sehemu hiyo.

Katika ombi lao kwa serikali ya Ujerumani wabunge wa vyama vya CDU,CSU na SPD wamesema sehemu hiyo ya mbuga ya wanyama ya Selous nchini Tanzania ni eneo kubwa kabisa na kongwe la hifadhi ya wanyama pori barani Afrika.

Wabunge hao wamesema mradi huo wa bwawa la nishati utahitaji sehemu kubwa sana itakayotokana na kukatwa kwa miti na hivyo kusababisha athari kubwa katika mazingira, tabia nchi na katika uchumi.

Wabunge wa chama cha upinzani cha FDP wameshauri kujengwa kinu cha nishati kutokana na gesi kwa sababu Tanzania inayo gesi ya kutosha iliyogunduliwa hivi karibuni. Chama hicho cha upinzani cha FDP kilichopinga azimio hilo kimeitaka serikali ya Ujerumani ifanye mazungumzo na serikali ya Tanzania.

Mwandishi/Zainab Aziz/Daniel Pelz/DW Berlin

Mhariri: Yusuf Saumu

Ujerumani: Mradi wa umeme wa Tanzania wapigiwa kura bungeni | DW | 18.01.2019
 
Maajabu kwelikweli,kuna watu watakuwa wamefurahia taarifa hii,lkn Stone alishasema hapangiwi na ukimpangia ndo umeharibu kabisa,pia alisema kuna watu hawafurahii huo mradi nazani wameshajotokeza, alishasema huo mradi lazima ujengwe!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
This is too much ila sio ya kustaajabisha sana. Hawa hawa wanaojadili masuala nyeti ya Tz kwenye bunge lao ndio wale wale walioandika katiba ambayo Tz imekuwa ikitumia kwa miaka zaidi ya hamsini iliyopita.
 
Unamaanisha Hii katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 imeandikwa na wajerumani?
I didn’t know you are that Ignorant, thank you.
 
Hilo nalo kweli maana ukisoma historia ya katiba ya Tanzania, wamekua wakiifanyia mabadiliko madogo madogo (amendments), imeshindikana kupata katiba mpya kama tulivyofanya sisi. Tatizo kila wakitaka kuibua mjadala, huwa wanalumbana kwenye suala la muungano hadi wanaachia.

Dah! Nimeshangaa sana eti bunge likae kujadili mradi wa nchi ya mbali, na wapate jeuri na ubavu wa kutoa mapendekezo ya huo mradi kupigwa chini, hainingii akilini, kuna kasoro sehemu. Hii dunia ina wenyewe, nimekubali leo, na haya ndio humkuta hata yule kiongozi wa Korea Kaskazini, yaani anatolewa maagizo na amri ya nini cha kufanya kwenye nchi yake. Japo yeye kidogo afueni, anaweza kutunisha misuli, hawa maskini wenzetu Afrika sijui itakuaje.
 
Mwenyewe nimeshangaa sana hili jambo..ila najua mzee baba hawezi kukubali hii dharau. Ila kama kutahadharisha tu hawa jamaa sio wenzetu kabisa wanaweza kutia figisu mpaka mradi uanze kujengwa hii ni pamoja kutia mkwara kampuni ya ujenzi na supplier wa materials .
 
This is too much ila sio ya kustaajabisha sana. Hawa hawa wanaojadili masuala nyeti ya Tz kwenye bunge lao ndio wale wale walioandika katiba ambayo Tz imekuwa ikitumia kwa miaka zaidi ya hamsini iliyopita.
Taahira wewe, katiba ya kikoloni inawezaje kutumika kwenye Taifa la kidemokrasia la kijamaa? Acha uchoko kudiscuss mambo yaliyokuzidi akili
 
Lengo lako wewe nikuwatoa povu watu. In short mkandarasi alishapatikana maamuzi ya bunge la ujerumani ni blind decisions hayata badili jambo lolote we have a strong president ever vitisho vimeshakuja vingi sana hakuna kilichobadilika
Baada ya kulipuliwa na wasomali juzi jamaa anatafuta pa kujifariji.
 
Hilo nalo kweli maana ukisoma historia ya katiba ya Tanzania, wamekua wakiifanyia mabadiliko madogo madogo (amendments), imeshindikana kupata katiba mpya kama tulivyofanya sisi. Tatizo kila wakitaka kuibua mjadala, huwa wanalumbana kwenye suala la muungano hadi wanaachia.

Dah! Nimeshangaa sana eti bunge likae kujadili mradi wa nchi ya mbali, na wapate jeuri na ubavu wa kutoa mapendekezo ya huo mradi kupigwa chini, hainingii akilini, kuna kasoro sehemu. Hii dunia ina wenyewe, nimekubali leo, na haya ndio humkuta hata yule kiongozi wa Korea Kaskazini, yaani anatolewa maagizo na amri ya nini cha kufanya kwenye nchi yake. Japo yeye kidogo afueni, anaweza kutunisha misuli, hawa maskini wenzetu Afrika sijui itakuaje.
Wamepiga chini kipi? Mbona mnajadili kimihemko bila kutumia uhalisia? Hilo bunge lilikua likishauri na kutoa mapendekezo kwa serikali ya ujerumani juu ya mradi wetu, na wakashauri serikali yao ifanye mazungumzo na serikali ya Tanzania kuhusu option ya kujenga kinu cha kufua umeme wa gas badala ya mradi wa Rufiji, na sio kama limetoa hayo mapendekezo yao kwa serikali ya Tanzania au kuzuia mradi usitekelezeke.
 
Toka bunge la Ujerumani linaloitwa Bundestag na maazimio yao kuhusu bonde la mto Rufiji, Tanganyika na mchango wa hoja za wabunge ktk bunge la Muungano la Tanzania huko Dodoma, Tanzania

Taahira wewe, katiba ya kikoloni inawezaje kutumika kwenye Taifa la kidemokrasia la kijamaa? Acha uchoko kudiscuss mambo yaliyokuzidi akili
Unamaanisha Hii katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 imeandikwa na wajerumani?
I didn’t know you are that Ignorant, thank you.
Hamfahamu hata historia ya nchi yenu? [emoji15] Kando na kufanya 'ammendments' kwenye katiba ya Tz. Chini ya mifumo mipya ya urais na hapo baadaye muungano na Zanzibar, watz hamjaandika katiba mpya tangu mpate uhuru kutoka kwa mkoloni.
 
Tanzania tuna msemo ,,shamba la bibi “ ukielewa asili ya huu msemo utaelewa uhusiano wa Ujerumani na Selous, hilo eneo lote lilikuwa mali ya Kaiser wa Ujerumani, Kaiser akamzawadia Mke wake hilo eneo lote kama zawadi ya birthday na, ndipo huo msemo ulipotokea, shamba la bibi, yaani eneo la Mke wa Kaiser.

Chanzo, kwetu ni Rufiji!

Hiki ni kioja kipya nakisikia leo 😂😂😂😂

Ngoja sasa nikupe maana halisi ya "shamba la bibi"

Maana ya bibi ni mama wa mama/baba yako

Msemo huo una maana kama shamba la wajukuu ambao wote hawana mamlaka au umiliki wake bali hutumia kigezo kwamba hili ni shamba la bibi yangu, kwa maana kama lingekua la mama/baba yake mmoja wao, mtoto wa baba/mama mwingine (mjomba) wake hasingeweza kwenda kulima sababu sio shamba la baba/mama yake kwa hiyo ni rahisi kufukuzwa lakini shamba la bibi hakuna wa kukufukuza zaidi ya bibi mwenyewe hivyo kila mjukuu atalitumia

Na ni hivyo sababu wabibi wanawapenda wajukuu wao wote na wabibi wengi huwa mashamba yao hulimwa sababu ya chakula cha wote na mengi ya mashamba ya wabibi huwa mapori sababu wabibi hawana nguvu ya kulima, nafikiri nimejaribu kukuelewesha kwa kiasi chake.

Unajua ni kwanini uwanja wa zamani wa Taifa huitwa shamba la bibi? Note, kila timu huwa ina uwanja wake wa club like msimbazi, chamazi, jangwani n.k
 
Hamfahamu hata historia ya nchi yenu? [emoji15] Kando na kufanya 'ammendments' kwenye katiba ya Tz. Chini ya mifumo mipya ya urais na hapo baadaye muungano na Zanzibar, watz hamjaandika katiba mpya tangu mpate uhuru kutoka kwa mkoloni.
Mungiki anapomfundisha mtanzania history 😂😂😂

Unajua hata German ilitawala lini Tanganyika kweli? Kwa hii pumba maana yake hata waingereza walikua wakiitumia katiba ya mjerumani, kunywa gongo taratibu bila kusumbua watu
 
Toka bunge la Ujerumani linaloitwa Bundestag na maazimio yao kuhusu bonde la mto Rufiji, Tanganyika na mchango wa Howard za wabunge ktk bunge la Muungano la Tanzania huko Dodoma, Tanzania

Sina uhakika na hili ila kuna nadharia inasema nchi ya Qatar ukubwa wake ni sawa na mkoa wa Dar. Kwa ufupi Dar ni kubwa! Sasa kukata miti kwa eneo lenye ukubwa wa Dar ni hatari kubwa! Tujaalie hata ukubwa wa hicho kisiwa cha Unguja ila bado ni eneo kubwa sana. Yaani kana kwamba hatuna njia nyengine mbadala.

Gas si tunayo! Binafsi tahadhari aliyoitoa Mh. Nape ni yenye faida na ushauri waliyotoa Bunge la Ujerumani ni mzuri. Mbali na hayo Selou ni miongoni mwa mbuga za Taifa, Ila Magu ni Rais mwenye akili za ajabu.
 
Back
Top Bottom