Afrika kazi bado ipo, nimeshangaa kwamba Tanzania bado ni koloni la Ujerumani

Afrika kazi bado ipo, nimeshangaa kwamba Tanzania bado ni koloni la Ujerumani

Sio mzuri wa historia lakini inasemekana hawa jamaa baada ya kushindwa vita ya kwanza ya dunia na kuporwa koloni na mwingereza asilimia kubwa ya mali zao walizifukia na kuondoka na ramani tu,mali hizo mpaka leo huwa wanaziiba taratibu.

Inawezekana hata kwenye hilo bonde kuna utajiri wao wanangoja muda tu kuuchota sasa huo mradi wanaona utawatibulia.
 
Nimesema katiba ni ile ile mlioachiwa na mkoloni, ambaye ni muingereza. Sijataja mjerumani popote. Azimio la arusha ndio ilikuwa ni katiba mpya? [emoji15] Aisee, MK254 muelimishe huyu Madenge kuhusu nchi yake. Anajifanya kwamba hanielewi hata kidogo. [emoji1]

Hakuna king'ang'anizi 'buku saba' yeyote unaweza kumuelimisha chochote, huwa hawaruhusiwi na wanakuwa monitored, akithubutu kuonyesha kulegea inamponza kiajira. Kwa hivyo anaweza kubisha ilmradi abishe tu, yaani hata kama mtakesha naye humu, hawa ni wa kuwapotezea.
Wakati unajadili naye uone ameanza kupinda, anatiririka pumba, hapo ndio unamuacha awe wa mwisho kujibu, usimjibu tena maana utakua unamtesa na kupoteza muda wako bure.
 
Hamfahamu hata historia ya nchi yenu? [emoji15] Kando na kufanya 'ammendments' kwenye katiba ya Tz. Chini ya mifumo mipya ya urais na hapo baadaye muungano na Zanzibar, watz hamjaandika katiba mpya tangu mpate uhuru kutoka kwa mkoloni.
Hahahaha, ninyi mlioandika katiba mpya, nini kimebadilika katika kutatua shida za wananchi ambazo ni
1)poverty
2)Unemployment
3)Corruption
4)Crime
5)Tribalism
6)Slums
7)gap BTW rich and poorer
8)Nepotism
9)Land distribution
10)Police killings

Au ninyi mnadhani kuandika katiba kwa ajaili ya kuongeza political posts na kuongeza mzigo wa kodi kwa mwananchi bila output yoyote ni ufahari?, mbona mnalalamika kwamba Punda amechoka?. Failed state nothing works.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
British wana uncodified constitution ambayo nyie mlioishia kusoma civics mnasema ni unwritten constitution. Though kihistoria the Magna carta of 1215 inatambuliwa kama part of documented Britain constitution. Samahan kwa kutumia lugha za kitaalam

Sent using Jamii Forums mobile app

Ahaaa haaa haaa
ndiyo mlivyofundishwa open university? tangu lini common law ikawa codified? unaposema uncodified law unamaanisha common law family ambayo asili yake ni uingereza.
codified ni civil law family which stems from Germanic law.

please kama siyo comparative lawyer and law philosopher bora upite kushoto.
 
Nimekutana na taarifa kwamba bunge la Ujerumani limekaa vikao kujadili mradi wa umeme wa Stiegler George kule Tanzania, na wakapiga kura ya kuupiga chini huo mradi. Hizi taarifa nimeshindwa kuzimeza maana zimenipa hasira, utani wa jadi pembeni, yaani wazungu wakalie vikao mradi ambao haupo hata kwenye bara lao huko Ulaya, kha Afrika kweli tuna shughuli, tena ndefu.

Maskini Watanzania, haya mjiandae kupokea amri kutoka kwa bwana mkuu, maana Mjerumani bado anawamiliki hata baada ya kusemekana kaachia enzi za ukoloni.
--------------------------------------

Ujerumani: Mradi wa umeme wa Tanzania wapigiwa kura bungeni
Bunge la Ujerumani limepitisha mswada wa kuitaka serikali ya Ujerumani itafute njia mbadala ya mradi wa Tanzania wa kuzalisha nishati ya umeme kwenye bonde la Stiegler ili kulinda turathi na asili.



Vyama vilivyomo katika serikali ya mseto ya Ujerumani vimeitaka serikali itafute njia nyingine badala ya ile ya mradi wa kuzalisha nishati ya umeme kwenye bonde la Stiegler kwenye mto rufiji kusini mwa Tanzania Wabunge wa vyama vya CDU/CSU, Kijani na AFD walishiriki katika kupiga kura hiyo lakini chama cha mrengo mkali wa kulia cha AfD, hakikushiriki. Azimio la vyama vya CDU,CSU na SPD pia linatokana na mapendekezo ya kamati ya serikali ya Ujerumani ya ushirikiano wa kiuchumi.
Azimio lililopitishwa bungeni na vyama hiyvo vilivyomo katika serikali ya mseto ya Ujerumani linaitaka serikali kuu isaidie katika masuluhisho ya kukidhi mahitaji ya nishati ya Tanzania bila ya kuathiri mazingira. Katika azimio lao vyama hivyo vimesema mradi huo mkubwa wa kuzalisha nishati ya umeme utavuruga mfumo wa mto mmojawapo mkubwa barani Afrika.

Tanzania inakusudia kujenga bwawa kubwa la kuzalisha nishati ya umeme kwa kutumia nguvu ya maji kutoka kwenye mto rufiji. Sehemu hiyo ni muhimu kwa shughuli za kilimo za wakaazi. Ikiwa mradi huo utaendelea mbele bonde la Stiegler ambalo limewekwa miongoni mwa turathi za shirika la Umoja wa mataifa la UNESCO litapoteza hadhi yake na huenda likasababisha athari kubwa katika raslimali zilizopo kwenye sehemu hiyo.


Katika ombi lao kwa serikali ya Ujerumani wabunge wa vyama vya CDU,CSU na SPD wamesema sehemu hiyo ya mbuga ya wanyama ya Selous nchini Tanzania ni eneo kubwa kabisa na kongwe la hifadhi ya wanyama pori barani Afrika.

Wabunge hao wamesema mradi huo wa bwawa la nishati utahitaji sehemu kubwa sana itakayotokana na kukatwa kwa miti na hivyo kusababisha athari kubwa katika mazingira, tabia nchi na katika uchumi.

Wabunge wa chama cha upinzani cha FDP wameshauri kujengwa kinu cha nishati kutokana na gesi kwa sababu Tanzania inayo gesi ya kutosha iliyogunduliwa hivi karibuni. Chama hicho cha upinzani cha FDP kilichopinga azimio hilo kimeitaka serikali ya Ujerumani ifanye mazungumzo na serikali ya Tanzania.

Mwandishi/Zainab Aziz/Daniel Pelz/DW Berlin

Mhariri: Yusuf Saumu


Ujerumani: Mradi wa umeme wa Tanzania wapigiwa kura bungeni | DW | 18.01.2019
Hawatatufanya lolote,na mradi utaendelea,wamepiga kura tu ili kujiridhisha,siye ni taifa huru
 
Hahahaha, ninyi mlioandika katiba mpya, nini kimebadilika katika kutatua shida za wananchi ambazo ni
1)poverty
2)Unemployment
3)Corruption
4)Crime
5)Tribalism
6)Slums
7)gap BTW rich and poorer
8)Nepotism
9)Land distribution
10)Police killings

Au ninyi mnadhani kuandika katiba kwa ajaili ya kuongeza political posts na kuongeza mzigo wa kodi kwa mwananchi bila output yoyote ni ufahari?, mbona mnalalamika kwamba Punda amechoka?. Failed state nothing works.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahaha...mkuu umesahau kumuuliza mbona katiba imeshindwa kuweka usalama wa taifa strong? Yaani Alshabab wanaingia Kenya na kufanya watakavyo as if ni Danguro,halafu yanapenda sifa makenya na kujitukuza hata kwenye hakuna
 
Unapozungumzia mito mikubwa Barani Africa hiyo ndiyo mikubwa...

1) River Nile - 6,650km
2) River Congo - 4,700km
3) River Niger - 4,200km
4) River Zambezi - 2,693km
5) River Ubangi - 2,270km
6) River Kasai - 2,153km
7) River Orange - 2,92km
8) River Limpopo - 1,800km
9) River Senegal - 1,600km

Alafu tuangalie:
River Rufiji unaousemea - 600km hichi ni ki-bwawa tuu

Tatizo bindamu wa siku hizi ni wabishi sana. Mnatetea hata ujinga.

Cc: mahondaw
Mito mikubwa kwa kipimo kipi?
 
Hayo ni mawazo yako
Hapa hakuna cha kupangiana ni cha kufanya project ya striglers rufiji
Inafanyika hakuna wa kuizuia!
Nyie mnataka tuendele kutumia umeme wa gas ili mtutoze malipo

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
😂😂😂😂 Nishamsoma kitambo hana hili wala lile me mwenyewe Nilikua nimemuandalia nondo za fundamental govern laws lakini nikaona ni kama nitapakia mzigo wa semi trailer kwenye tray la mayai, I reserved.

Ahaaa haaa haaa
yule mwanasheria mwitu Ibofwee mbona simuoni, kakimbilia wapi?

Ahaaa haaa haaa
😂😂😂😂
 
Hawa wazungu wababaishaji tu.wskati nchi inapata shida ya UMEME miaka ya karibuni binge lao halikukaa kutushsuri kujenga mfumo WA mkubwa WA UMEME WA gesi.Leo tunataka kuzalisha meg 2100 wanatoa mswazo .pigs chini mawazo yao .UMEME WA rufiji mbele kwa mbele TZ oyee
 
Sina uhakika na hili ila kuna nadharia inasema nchi ya Qatar ukubwa wake ni sawa na mkoa wa Dar. Kwa ufupi Dar ni kubwa! Sasa kukata miti kwa eneo lenye ukubwa wa Dar ni hatari kubwa! Tujaalie hata ukubwa wa hicho kisiwa cha Unguja ila bado ni eneo kubwa sana. Yaani kana kwamba hatuna njia nyengine mbadala.

Gas si tunayo! Binafsi tahadhari aliyoitoa Mh. Nape ni yenye faida na ushauri waliyotoa Bunge la Ujerumani ni mzuri. Mbali na hayo Selou ni miongoni mwa mbuga za Taifa, Ila Magu ni Rais mwenye akili za ajabu.
kila kitu kina negative effects ..... hata dawa unazo kunywa pia zina negative effect zake... ko unacho pima ni faida ..kma umesoma uchumi au japo kupitia maswala ya kiuchumi kwa umakini utakua umepata picha ya ninacho ongea..mfano una eneo lako kama hekari moja una options mbili kulima mboga mboga na kulima miti... ukitumia robo ya eneo kulima mboga mboga basi robo tatu utalima miti and vice versa....sasa hapo utaangalia faida na hasra za machaguzi yako...kwa makadilio yangu mladi utalipa maana umeme huo tutakuwa na uwezo wa kuuza hata nchi za jirani
 
Back
Top Bottom