MtamaMchungu
JF-Expert Member
- Apr 10, 2011
- 10,115
- 15,057
Ndio wavunjaji wakuu wa sheria za kimataifa, wangejaa huko kama wangekuwa membersKwanini Marekani hawaitaki hii mahakama?ni zipi sababu zao za msingi?
Umewahi kuwa victim wa serikali/wanasiasa?Kuuwawa kumeanza kuwepo kabla mama yako hajazaliwa.
Wameuwawa watu enzi za Yesu kwa kukatwa vichwa wewe unashangaa watu kuuwawa leo.
Umeshasahau kuwa kibiti na Mkuranga watu waliuwawa! Au vifo vyao havina umuhimu?
Wanauwawa watu Msumbiji kila siku bila ya hatia au wao sio muhimu?.
Umeongea upuuzi, kama icc wamethubutu kutaka kushitaki hao wanajeshi wa marekani kwanin unasema eti icc ipo kwa afrika tu?NI KAMA USHAMBA TU LEO AFRIKA KUSHABIKIA ICC?
Na Elius Ndabila
0768239284
Msamiati wa ICC umekuwa maarufu sana Tanzania kwenye uchaguzi wa mwaka huu. Ninaamini wapo ambao wanalitamka neno ICC wakiwa wanalijua vizuri na wapo ambao wameingia tu kwenye mkenge bila kujua. Leo nitawapitisha kidogo juu ya ICC ili tujue kama ni USHAMBA au ni Ujuvi kuendelea kushabikia hili.
Kwanza ICC(International Criminal Court) ni Mahakama iliyoanzishwa mwaka 2000 huko Rome kwa madhumuni ya kushitaki mauji ya Kimbari, hatia dhidi ya binadamu na hatia za kivita. Ilianzishwa baada ya majadiliano ya takilibani miaka mitatu.
Hii ndiyo ilikuwa tafsiri ya Mahakama hii. Lakini ukweli wa mambo ni kuwa kuanzisha Mahakama hii ilikuwa ni akili kubwa ya Wazungu hasa waliokuwa na makoloni Afrika mwanzoni kutafuta mbinu mbadala ya kuendelea kuikalia Afrika kusaidiana na ukoloni Mambo leo. Waasisi wa hii Mahakama ni Ujerumanj ambayo ikumbukwe ilipitia kwenye misukosuko ya kiuchumi kwa mda mrefu baada ya bara la Afrika kuwa huru.
Ujerumani kushirikiana na Uingereza ndio walishikia bango kuanzisha kwa Mahakama hii kwa kuwa wao walikuwa na madhumuni makubwa mbali na yale yanayotajwa kwenye Rome Statutes. Wakati wa uanzishwaji nchi 34 za Afrika zilisaini, Ulaya 25 na visiwa vya Caraibean na Amerika 28 nazo zikijiunga.
Wakati mataifa hayo yakijiunga mataifa makubwa ambayo yalishajua kuwa lengo la Ujerumani, Uingereza na wafuasi wao ni kutaka kuendelea na ukoloni wao walikata kujiunga na Mahakama hiyo. Mataifa yaliyokata ni Marekani, China, Urus n.k ndiyo maana pamoja na Marekani kutuma Wanajeshi wake kuua, lakini haijawahi kushitakiwa kwa kuwa si wanachama wa Mahakama hii.
Kumbukumbu zinaonyesha tangu Mahakama hii kuanzishwa yaani miaka 20 sasa ICC imechunguza kesi 26 nyingi zikiwa bado ktk awamu ya majaribio, imetoa waranti 32 za kukamatwa, 15 zikitekelezwa na ina wafungwa 6 ambao wote wanazuiwa. Hukumu ya Kwanza ilikuwa ni mwaka 2014 tangu kuanzishwa. Kesi karibia zote zinatoka Aftika. Kitendo hiki ndicho kinatoa taswira kuwa Mahakama hii ilianzishwa kwa ajili ya bara la AFRIKA ambapo Mahakama hii imekuwa ikitumiwa na Wabaya wa nchi za Afrika kuzishitaki hasa pale wanapoona kiongozi aliyeshinda kwenye uchaguzi hata kidhi mahitaji yao ya kulinyonya bara la AFRIKA.
Ni Mahakama ambayo kwa nchi wanachama inatumika kama chambo cha ukadamizaji hasa unaposhindwa kutii matakwa yao. Ni Mahakama inayotoa vikwazo hasa economic sanction kwa nchi zinazoshindwa kufuata matwa yake.
Ukweli ni kuwa ili Afrika iweze kusonga mbele inahitaji kuwa na nguvu ya pamoja katka kutatua mambo yao. Duniani kote sasa wanaitegemea Afrika kwa rasilimali ya viwanda vyao. Sasa kazi kubwa ambayo sasa mataifa makubwa yanafanya ni kuhakikisha kuwa Afrika Wanafarakana, ni kuhakikisha kuwa wanatengeza makundi ndani ya nchi yatakayoleta misuguano ambayo itawarahisishia wao kupenyeza agenda zao. Mahakama hii imemezwa na bunge la EU.
Mwaka 2018 Rais wa Marekani Mh Donald Trump alitishia kupeleka hoja ya kuifuta Mahakama hii kandamizi. Na kwa kuonyesha u serious wa hilo waziri wa Mambo ya Kigeni Mh Mike Pompeo alitangaza kuwawekea vikwazo viongozi wa Mahakama hiyo wakiongozwa na MwanaMama Fatou Besouda waliokuwa wanajaribu kutishia kuwa wangeeashitaki wanajeshi wa Marekani.
Imefika mahali Waafrika tuamuke. Tuache usingizi wa akina Mangungo. Mahakama hizi hazina upendo na sisi Bali kwenye kutimiza matakwa yao. Ingekuwa ni Mahakama ya haki mungekuwa mnasikia na wao wanashitakiwa, lakini ile ni Mahakama ya Afrika ili kuendelea kutukandamiza. Tunayofursa ya kulijenga bara la AFRIKA kuwa zaidi ya Ulaya kwa kuwa tunazo rasilimali za kutosha kufanya hivyo. Tukiendelea kuwashobokea tutakuwa masikini milele, na watakomaliza kuvuna rasilimali zetu watatua vumbi.
Tafakari.
Nafuata sheria kadri ya uwezo wangu wote, kadri niwezavyo.Umewahi kuwa victim wa serikali/wanasiasa?
Vizuri.... wewe unadhani kila anayeumizwa na wanasiasa hakufuata sheria?Nafuata sheria kadri ya uwezo wangu wote, kadri niwezavyo.
Serikali inafanya kila liwezekanalo kulinda raia wake.Vizuri.... wewe unadhani kila anayeumizwa na wanasiasa hakufuata sheria?
Unadhani wananchi wa Congo Mashariki wooote ni wahalifu?
Unadhani wananchi wa Darfur wooote ni wahalifu?
Au Wakenya walioathirika na vurugu za baada ya uchaguzi 2007 walikuwa hawafuati sheria?
ICC kazi yake ndio hiyo, kuwapatia haki watu ambao serikali zao hazina uwezo au nia ya kuwapa haki. Tusiangalie sana kuhusu Marekani na Ulaya, tuwaze kuhusu sisi, leo hii ikitokea Serikali imeanza kudhuru raia wake, wewe unadhani utaenda wapi kupata haki?
Ukiona mtu amekuwa verified user ujue ni takataka na ataandika takataka. Unadhani kuna mtu atakupigia simu?
Vizuri.... wewe unadhani kila anayeumizwa na wanasiasa hakufuata sheria?
Unadhani wananchi wa Congo Mashariki wooote ni wahalifu?
Unadhani wananchi wa Darfur wooote ni wahalifu?
Au Wakenya walioathirika na vurugu za baada ya uchaguzi 2007 walikuwa hawafuati sheria?
ICC kazi yake ndio hiyo, kuwapatia haki watu ambao serikali zao hazina uwezo au nia ya kuwapa haki. Tusiangalie sana kuhusu Marekani na Ulaya, tuwaze kuhusu sisi, leo hii ikitokea Serikali imeanza kudhuru raia wake, wewe unadhani utaenda wapi kupata haki?
Mbona wamarekani wameua sana tu hapo Uarabuni tena wakina mama na watoto lakini hawajashitakiwa? Nisaidie mkuu ili nielewe!
Ndugu unaongea kama vile unaishi kwenye kisiwa. Unalolisema ni wakati zinatimiza wajibu wake, ICC ipo kwa ajili ya serikali au viongozi wanaokwenda kinyume.Serikali inafanya kila liwezekanalo kulinda raia wake.
Lakini inaundwa na binadamu wenye udhaifu wa kila aina, lengo la jumla ni jema ingawa upungufu haukwepeki.
Kama hayo ni makosa na yako ndani ya Rome Statue, wakashitakiwe. Uzuri wa ICC hata wewe unaweza kwendaunapozungumzia haki za binadam, ni pamoja na wale waliofukuzwa bungeni kipindi cha corona pia, na wale wanaotishiwa maisha wakitaka kua wenyekiti, haki za binadam sio kuuliwa tu
Ndio maana huko nyuma nimeuliza nani atampeleka Trump huko ICC? Maana kasababisha mpasuko mkubwa US.Ndugu unaongea kama vile unaishi kwenye kisiwa. Unalolisema ni wakati zinatimiza wajibu wake, ICC ipo kwa ajili ya serikali au viongozi wanaokwenda kinyume.
Nimekupa mfano wa Darfur, labda nikuulize watu waliopata madhara huko haki wakapate wapi?
Mkuu mleta mada, humu jukwaani kuna Mawakala wa Wazungu wao kazi yao ni kuwatisha Watanzania.
Ni marafiki wa yule kaka wa MIGA, wameshindwa kabisa kuelewa kuwa awamu hii ni ya kizalendo na isiyokuwa na uoga wa kuyatetea maslahi mapana ya nchi.
Kenya kulikuwa na vita ya dhahiri ya kiukabila na walikufa watu zaidi ya elfu moja.
Lini Tanzania imetokea vita ya uchaguzi mpaka wakafa watu elfu moja, hatuna siasa za kiukabila wala za kimajimbo kama Ethiopia ya sasa.
Wapo mawakala wa wazungu wanajaribu kuivuruga hii nchi lakini hawataweza kwani ina misingi imara sana.
Wazalendo halisi lazima tuitetee TZ dhidi ya madalali wa wapigaji wa rasilimali zetu.Wazalendo uchwara co?wa kusifu na.kuabudu
Wazalendo halisi lazima tuitetee TZ dhidi ya madalali wa wapigaji wa rasilimali zetu.