Afrika Kusini: Jamii Forums yasifiwa kufanya kazi kwa weledi

Afrika Kusini: Jamii Forums yasifiwa kufanya kazi kwa weledi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mail & Guardian moja kati ya gazeti linalopigania usawa na uhuru wa kujieleza katika nchi za Kiafrika limeandika kuwa Uandishi wa Habari unapoteza maana yake kwa kuwa waandishi wa habari wana Uanaharakati na urazini katika uandishi wao.

Wameandika kuwa ni vyombo vichache ambavyo hufanya kazi kwa weledi bila kuonesha upanede wanaoegemea ambao katika hilo wameitaja Jamii Forums na kutoa mfano wa namna ambavyo Uchaguzi Mkuu ulivyoripotiwa, aidha wamekitaja pia Premium Times cha Nigeria kwa kile kilichoripoti kuhusu EndSARS.

Katika makala yao waliyoipa jina la “Journalists have to be seekers of Truth, not activists” wameandika mambo mengi ambayo yanaonesha taaluma ya habari haichukuliwi kwa msingi wake bali inachezeshwa chini ya kiwango kutokana na waandishi kufanya mambo yasiyoweza kujenga, kwa kiasi kikubwa wamesema waandishi wamekuwa wakiwapa watu vitu wanavyotaka kuvisikia/kuviona badala ya kuwapa vitu vya kweli.

Imeandikwa kuwa vyombo vya habari ni kitu kikubwa katika kuleta mabadiliko katika nchi wakitoa mfano wa mwanasheria wa Ethiopia aliyeacha kuwa wakili na akawa mwanahabari baada ya kutambua kuwa haki inaweza kupatikana hata nje ya mahakama.

Soma makala kuhusu uandishi wa habari iliyoandikwa na Mail & Guardian Hapa
 
Daah lakini Ile condition discharge aliyopigwa Melo....inafikirisha!
 
Mwisho wa kufanya kazi kwa weredi ilikuwa jana...kuanzia leo ni kunyooshwa tu..
 
Back
Top Bottom