Leo nchi vinara wa uchumi wa Afrika wanaandamana kudai maisha bora, demokrasia na utawala bora. Inashangaza nchi hizi ambazo zina unafuu ukilinganisha na Tanzania katika masuala ya maendeleo wapo barabarani wanadai mambo bora zaidi.
Maandamano ya amani ni njia mojawapo nzuri sana ya kudai yote yale tunayohitaji serikali yetu itufanyie. Ni njia nzuri ya kufikisha ujumbe kwa viongozi wetu endapo njia za kawaida zimeshindikana. Huu ni wakati wa vuguvugu la ukombozi wa Afrika dhidi ya serikali zisizojali matakwa ya raia wake.
Naelewa kuwa JPM aliwaogofya watanzania kwa staili ya uongozi wake uliojaa ukatili kiasi kwamba miaka miwili baada ya kifo chake bado tumeendelea kufikiri tupo chini ya mfumo wake.
Je watanzania tuna haja ya kuandamana kudai unafuu katika kodi, tozo, pembejeo za kilimo na hata katiba mpya na tume huru ya uchaguzi? Pengine huu ndio wakati mzuri wa kuleta mabadiliko hayo kwa mshikamano wetu.