Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Mawakili wa kiongozi wa Chama cha Economic Freedom Fighters (EFF), Julius Malema, wamewasilisha maombi wakati mchakato wa utoaji hukumu kwa kiongozi huyo ulipoanza katika Mahakama ya Hakimu KuGompo, katika eneo la Eastern Cape, leo Jumatano Aprili 15, 2026.
Hakimu Twanet Olivier amesikiliza hoja za mwisho kutoka kwa upande wa utetezi na upande wa mashtaka kabla ya kuahirisha shauri hilo hadi kesho asubuhi Alhamisi Aprili 16, 2026 kwa ajili ya kutoa hukumu.
Mwendesha mashtaka Joel Cesar ameiambia mahakama kuwa anaomba Malema apewe kifungo cha hadi miaka 15 jela, baada ya kupatikana na hatia Oktoba 2025 kwa makosa matano chini ya Sheria ya Udhibiti wa Silaha za Moto.
Soma Pia: Julius Malema akutwa na hatia ya kutumia silaha hadharani, aweza kufungwa miaka 15
Aidha, ameomba adhabu ya kifungo cha miaka 10 jela, ambapo miaka mitatu itasimamishwa, pamoja na faini kwa makosa yaliyosalia.
Mashtaka hayo yanatokana na tukio la mwaka 2018 katika mkutano wa EFF huko Mdantsane, ambapo Malema alifyatua risasi hewani. Mshtakiwa mwenza, Adriaan Snyman, aliachiliwa huru.