Afrika Kusini: Meja Jenerali apigwa risasi na wasiojulikana siku kabla ya kutoa ushahidi kesi ya Ufisadi

Afrika Kusini: Meja Jenerali apigwa risasi na wasiojulikana siku kabla ya kutoa ushahidi kesi ya Ufisadi

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Meja Generali Polisi Feroz Khan, ambaye amesimamishwa kazi kama naibu mkuu wa kitengo cha ujasusi wa makosa ya jinai, alijeruhiwa katika shambulio hilo la Juni 28, 2026, akiwa njiani kuelekea nyumbani kwake. Shambulio hili limetokea siku chache tu kabla ya kiongozi huyo kufika mbele ya kamati kuu ya uchunguzi inayoshughulikia madai ya ufisadi na mitandao ya uhalifu ndani ya jeshi la polisi nchini humo.

Mamlaka zimeanzisha uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo. Hata hivyo, msemaji wa polisi, Brigedia Athlenda Mathe, ametoa mwito wa kuwa waangalifu na kutokurupuka kuhusisha shambulia hilo na ushahidi ambao Khan alipaswa kuutoa mbele ya Tume ya Madlanga.

Tume hiyo iliundwa kufuatia madai mazito yaliyotolewa na Luteni Jenerali Nhlanhla Mkhwanazi kwamba makundi ya wahalifu yameingilia na kusambaa kwenye baadhi ya idara za serikali na vyombo vya usalama.

Khan alikuwa miongoni mwa watu walioitwa kutoa ushahidi baada ya jina lake kutajwa kwenye vikao vya awali. Alitarajiwa kuhojiwa kuhusu operesheni ya madawa ya kulevya iliyofeli mwaka 2021 mjini Johannesburg, pamoja na madai yaliyoripotiwa na vyombo vya habari kuhusu uhusiano wake na kiongozi wa upinzani Julius Malema na mwanasiasa Brown Mogotsi.

Mapema mwezi huu, Khan alijaribu bila mafanikio kuzuia wachunguzi wasikague vifaa vyake vya kielektroniki vilivyokamatwa wakati alipotiwa mbaroni. Pia alikuwa ameomba ushahidi wake usikilizwe faragha kabla ya kuondoa ombi hilo baadaye.

Shambulio hili linazidisha hofu inayozidi kukua kuhusu usalama wa watu wanaohusishwa na uchunguzi huo. Mnamo mwezi Desemba, shahidi mwingine aliyekuwa akihusiana na tume hiyo aliuawa mbele ya ndugu zake, wiki chache tu baada ya kufika mbele ya wachunguzi.

Khan alikamatwa mwezi Mei akiwa na afisa mwingine mkuu wa polisi pamoja na mfanyabiashara mmoja, katika kesi inayohusisha madai ya biashara haramu na umiliki wa dhahabu.

Mashitaka hayo yanatokana na tukio lililotokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa OR Tambo mjini Johannesburg mwaka 2021, ambapo mamlaka zilimkuta mfanyabiashara mmoja akiwa na karibu gramu 76 za dhahabu ambayo haijasafishwa. Kulingana na wachunguzi, mfanyabiashara huyo alidai kuwa alikuwa akifanya kazi ya siri kwa niaba ya viongozi wakuu wa jeshi la polisi.

Hadi sasa, Khan hajazungumza chochote hadharani kuhusu madai yanayomkabili wala kuhusu shambulio hilo la risasi.

1782801517465.png

Major General Feroz Khan​

Soma pia

===========

A senior South African police official has been hospitalised after gunmen opened fire on his vehicle in Johannesburg, days before he was expected to appear before a high-profile inquiry into alleged corruption and criminal networks within the country's police service.

Major General Feroz Khan, the suspended deputy head of crime intelligence, was wounded in the attack on Sunday evening while travelling home. Reports in local media said he underwent emergency surgery.

Authorities have launched an investigation into the incident. Police spokesperson Brigadier Athlenda Mathe urged caution over suggestions that the shooting was connected to Khan's scheduled testimony before the Madlanga Commission.

The commission was established following explosive claims by Lieutenant General Nhlanhla Mkhwanazi that organised crime had infiltrated parts of the state and law enforcement agencies.

Khan was among those called to give evidence after his name surfaced during proceedings. He was expected to face questions over a failed 2021 drug operation in Johannesburg, as well as allegations reported by local media concerning his relationship with opposition leader Julius Malema and political figure Brown Mogotsi.

Earlier this month, Khan unsuccessfully sought to prevent investigators from examining electronic devices confiscated during his arrest. He had also requested that his testimony be heard in private before later withdrawing the application.

The attack adds to growing concerns around the safety of individuals linked to the inquiry. In December, another witness connected to the commission was killed in front of relatives weeks after appearing before investigators.

Khan was arrested in May alongside a fellow senior police officer and a businessman in a case involving the alleged unlawful trade and possession of gold.

The charges relate to an incident at Johannesburg's OR Tambo International Airport in 2021, where authorities found a businessman carrying nearly 76 grams of unrefined gold. According to investigators, he claimed he was working undercover on behalf of senior members of the police service.

Khan has not responded publicly to either the allegations against him or the shooting.


Source: African news
 
Back
Top Bottom