Afrika Kusini na Misri tu hatujazifikia hata kwa 25% je, hizo London, New York na Paris ndiyo tutazifikia haraka?

Afrika Kusini na Misri tu hatujazifikia hata kwa 25% je, hizo London, New York na Paris ndiyo tutazifikia haraka?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
“Nataka Tanzania iwe kama Ulaya, nataka Nchi hii iwe kama Ulaya, sisi ndio tuwe tunatoa misaada na mipango hiyo tunayo na mipango hiyo imepangwa vizuri kupitia Ilani ya CCM” -JPM

East Africa Television - News

Kama Kauli hii imetolewa tu 'Kisiasa' zaidi kuelekea katika Kampeni za Uchaguzi huu ujao wa 2020 naikubali, ila kama ni ya Kweli ninamkatalia JPM.
 
Ngoja niagize popcorn nisubiri maoni ya wachangiaji. johnthebaptist. njoo huku ujibu swali.
 
Yaani hata mimi huwa nashangaa ninaposikia waimba mapambio, wanavyojisifia na kujilinganisha!!!!!
 
Rais analenga waliopo juu zaidi tukiikosa ulaya basi tutawazidi Misri na South Africa

Kuliko kuitarget South Africa halafu ukiikosa target unaishia kuwa kama Msumbiji..

Aim for the stars.
.
 
Hakuna Kitu ambacho GENTAMYCINE nakichukia katika Maisha yangu kama Uwongo na Unafiki. Ili uitamani Namba 10 kwanza itamani Namba 2.
Kwa aina ya mipango tuliyo nayo kama taifa hata miaka 100 hatuioni Afrika ya kusini maana tunaamini katika vitu hatujawekeza katika watu (ELIMU,KILIMO AFYA) Ndio mhimili mkuu wa maendeleo mengine ni mbwembwe tu
 
Kufikia maendeleo ya uchumi wa juu ni swala la mchakato 2025 tunapaswa kuifikia per capita ya $ 3000!
Huu ni uongo niambie ni sekta gani ambayo serikali imewekeza ili kufika hilo lengo, ili ufikie maendeleo lazima uwekeze katika watu kwenye Elimu, Kilimo na Afya haya yote mmeyatupa kapuni mmewekeza katika miundombinu tu na kuacha 85% hawajui hata kesho yao.
Tuwe wazalendo ukweli daima Tanzania ni yetu wote
 
Back
Top Bottom