Jana na juzi kitengo cha Propaganda cha CCM kilizua taarifa kuwa Rais wetu wa Tanzania amepewa tuzo ya amani ya Nelson Mandela. Mitandaoni na baadhi ya vyombo vya habari vikalitaja tukio hilo kwa sifa na mapambio wakati wewe Polepole na watumishi wako wa propaganda mkijua sio kweli na ni kumfedhehesha Rais kama mlivyofanya kwenye Tuzo ya FORBES na eti Trump wa US kamsifia kwa barua Rais.
Mjue mnapomtaja Rais ni kuwa mnaizungumzia Tanzania na aibu inakuwa ya nchi kwetu sote. Next time mkitaka kutangaziana vitu fake basi Polepole tunakuasa uandike hivi
"MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI JOHN MAGUFULI KATUNUKIWA TUZO YA so and so" ili hiyo aibu ya kujulikana ni uongo ibaki huko kwenye chama chenu mlicho zoea kudanganya na haitaihusu nchi.