Afrika Kusini: Wakristo na baniani waandamana wakitaka adhana

Afrika Kusini: Wakristo na baniani waandamana wakitaka adhana

Dah ...wengine hiyo ndiyo hutuamsha asubuhi "tupashe" [emoji2960]
Dada mmoja jirani yangu ni mfanyabiashara wa kuwahi soko mapema.Sisi tukisikia adhana twajitayarisha kwenda msikitini na yeye tunakutana njiani anawahi sokoni.Anajua akisikia adhana ni muda wa watu wema kuingia barabarani na vibaka kupumzika.
 
Adhana hua inachukua muda gani? Sidhani hata kama inafika dakika 4
Vipi kuhusu makelele yanayopigwa kwenye ma Bar?
Kama hutaki makelele nenda ukaishi peke yako huko porini,kelele ni dalili ya uhai na haziepukiki.
Hizo dk 4 ni kero kubwa sana.

Kama unajua muda wa kwenda kuswali, usisubiri uitwe na adhana.

Weka alarm.
 
Nadhani adhana haiwezi kuingia kwenye kundi la makelele.Sijui kamusi la kiswahili linasemaje lakini naona kama makelele ni maneno yasiyo na mpangilio maalum wala faida yoyote kwa anayesikiliza.
Kelele ni sauti unazosikia halafu huzihitaji.

Ukiwa karibu na bar wanapiga mziki, hizo ndo kelele.

Huhitaji kusikia hizo kelele.
 
Hizo dk 4 ni kero kubwa sana.

Kama unajua muda wa kwenda kuswali, usisubiri uitwe na adhana.

Weka alarm.
Mungu anatuhurumia sana waja wake,na sisi ni muhimu kuzinduka kwa hilo na kuhurumiana wenyewe kwa wenyewe.Adhana imeletwa ili iwe ni ukumbusho wa mtu kwenda kuswali,ipo fupi tu na maneno yenye maana kubwa na kwa sauti nzuri,Inarudiwa mara kwa mara ili iwe ushahidi kwamba ulikumbushwa ili litakalokukuta huko mbele ujilaumu mwenyewe na si kumlaumu Mungu wala majirani zako.Huko mbele kuna hali ngumu sana kwa aliyedharau mwito.
Hizi dakika nne mara tano kwa siku si chochote katika wakati wako unaoutumia kwa siku kufanya mambo mengi maovu ambayo yote ni kwa faida ya shetani.
 
Waandamanaji wenyewe wanaonekana wahuni tu wala Kanisa hawalijui, Adhana ni lazima ziwe regulated ni kelele sana
 
Waandamanaji wenyewe wanaonekana wahuni tu wala Kanisa hawalijui, Adhana ni lazima ziwe regulated ni kelele sana
Dalili gani kuwa ni wahuni,mbona wamekaa vizuri.Tatizo hawana akili kama zako.
 
Dada mmoja jirani yangu ni mfanyabiashara wa kuwahi soko mapema.Sisi tukisikia adhana twajitayarisha kwenda msikitini na yeye tunakutana njiani anawahi sokoni.Anajua akisikia adhana ni muda wa watu wema kuingia barabarani na vibaka kupumzika.
Kwa enzi hizi za Teknolojia adhana hazina Tena umuhimu huo, Ni Kama kutegemea jogoo akuamshe, wakati Kuna simu za Bei rahisi unaweka alarm muda wowote unaotaka
 
Adhana inalengo lakuwaamsha wanaotaka kwenda kuswali lakini hata wasiotaka kwenda kuswali wanaamshwa pia hivyo kwao inakua ni usumbufu.
Kwateknolojia ya sasa nashauri waumini waweke alarm zenye adhana na tatizo litakua limeisha.

Sent from my Infinix X603 using JamiiForums mobile app
 
Mjifunze sasa upendo wa wenzenu katika imani yenu. Nyie kutwa kuwaita wenzenu makafiri na kuwafundisha hadi watoto kuchukia imani zingine nje ya uislam na mnawafundisha watoto kuita dini zingine makafiri.... halafu makafiri hao hao wanawakingia kifua inapotokea mnakandamizwa....
 
Kwa enzi hizi za Teknolojia adhana hazina Tena umuhimu huo, Ni Kama kutegemea jogoo akuamshe, wakati Kuna simu za Bei rahisi unaweka alarm muda wowote unaotaka
Hii dhana ya kwenda na teknolojia kwa kila jambo haiko sawa.Ziko teknolojia nyingi za kizamani ambazo wala hazitapitwa na muda wake. Na ziko teknolojia za kisasa zina madhara makubwa na wala hazina ulazima.Mfano ni hiyo alarm kuchukua nafasi ya adhana.Kwanza kwa madhumuni ya adhana alarm haihitajika na pili alarm inaumiza mishipa ya fahamu na inaweza ikaleta ugonjwa wa moyo ikiwa itatumika kila siku.Gari moshi au treni ni teknolojia ya zamani lakini kila siku zinavyokwenda mbele nchi nyingi zimeona ni suluhisho la usafiri kwenye miji mikubwa.
Adhana tumesema ni ukumbusho ili kila mtu umfikie na ni kwa faida ya huko tuendako akhera.Katika majuto mkristo asije akamlaumu muislamu kwa kutokumuongoza kuujua uislamu na muislamu asije akamlaumu muislamu mwenzake kwa kutokumuhimiza kwenye ibada.
Ukiwa ni mkristo ni muhimu kujiuliza na kuzingatia ni sauti gani hii nzuri kila siku inayotoka misikitini huenda ukazinduka.
 
Nyumba za ibada zisiwe chanzo cha kelele zisizo na tija.

Wafunge maspika yao ndani na kelele zisitoke nje.

Utakuta kanisa moja linapiga kelele mtaa mzima au msikiti mmoja wanapiga kelele mpaka mtaa wa 3 unasikia.

Hii tabia ikome.
Sanaaa
 
Mimi nikikaa sehemu haina adhana naonaga short kabisa kama sipo Tanzania...waache watu waitane kwenye ibada zao


Adhana ni moja ya utambulisho wa Tanzania---- inatambulisha kwamba hapa upo Tz.

The point noted.
 
Hizo dk 4 ni kero kubwa sana.

Kama unajua muda wa kwenda kuswali, usisubiri uitwe na adhana.

Weka alarm.


Katika uisilamu hakuna mbadala wa adhana, mfano katika uisilamu kabla hujaswali ni lazima utawadhe/uchukue udhu kwa maji safi lakini kama maji hayapo au ni ya shida au kwasababu yoyote mtawadhaji hawezi kuyatumia basi uisilamu umetoa mbadala wa "tayammam" yaani kutawadha kwa kutumia mchanga uliokuwa safi au kama mchanga safi hakuna basi apangushe mikono yake kwenye ukuta, meza au kitu chochote kilichokuwa safi na afanye "tayammamu"--- kupangusa mikono usoni mara moja na tena kupangusa mikononi mara moja, hiyo ndio mbadala wa kutawadha katika uisilamu, kinyume chake hakuna mbadala wa adhana, lazima itolewe kwa sauti ili iwafikie watu na waende kuswali, adhana licha ya kuwaita watu kuswali lakini pia ni nasaha kutoka Mungu kwa watu wote isitoshe ni sehemu ya ibada muhimu kuliko ibada zote ibada ya swala hivyo kuzuia adhana ni kuhafifisha ibada muhimu ya swala, Kuabudu ni uhuru wa kila mtu kikatiba.
 
Nendeni mkaandamane Rwanda kagame amepiga marufuku hizo kelele zenu zisizo na tija
 
Tija usioijua wewe.Usizuie wengine kupata hiyo tija.Inabidi uvumilie,
 
Back
Top Bottom