Afrika: Kwanini Al Ahly wanacheza CAF CL?

bulabo

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2015
Posts
628
Reaction score
780
Afrika inachekesha sana kwa kigezo gani Al ahly wanashirik CAF CL hii ndio maana soka letu Afrika linashida kubwa.
 
1. CAF waliomba nchi wanachama wote wapeleke majina ya timu zitakazocheza CL na CC kila mwanachama kwa idadi yake na wakatoa deadline ya kupeleka majina hayo

2. Deadline ya kupeleka majina iliyowekwa na CAF ilikuwa ni muda ambao ligi ya misri ya msimu huo ilikuwa haijamalizika

3. Kwa kuliona hilo, chama cha soka misri kikapeleka majina ya waliokuwa wanaongoza ligi kufikia mwisho wa raundi ya kwanza ya ligi

4. Hivyo, kigezo kilichotumika ni msimamo wa ligi kwa raundi ya kwanza, yaani nusu msimu wa ligi na sio msimamo wa ligi baada ya ligi kuisha

Hicho ndicho ninachokijua mimi, kama
 
Waliopeleka wawakilishi ni FA ya Misri nafikiria walifanya upendeleo kwa kuangalia rekodi yao ila pyramid walitishia kwenda CAS ngoja tuone mwisho wake
 
Afrika inachekesha sana kwa kigezo gani Al ahly wanashirik CAF CL hii ndio maana soka letu Afrika linashida kubwa.
Nilitegemea usubiri jibu la swali kabla ya kubeza kwamba soka la Afrika lina shida. Shukrani kwa Sima70 ambaye ametoa majibu mazuri na kwa mpangilio mzuri.

NB: Kuna kipindi Mwina Kaduguda akiwa Katibu Mkuu wa FAT aliamua kupeleka majina ya Simba na Mtibwa kushiriki michuano ya CAF baada ya kuona ligi ya Muungano (wakati huo ndio inatoa wawakilishi) itachelewa deadline, na CAF wakayapokea
 
Mbadala unadhani kilitakiwa kifanyike kitu gani na deadline ilikuwa unakaribia kufikiwa?
 
Al Hilal ni timu kubwa..hata Tanzania ikija kutokea mazingira kama hayo TFF wala haitahangaika itapeleka jina la .....
 
Nilitegemea usubiri jibu la swali kabla ya kubeza kwamba soka la Afrika lina shida. Shukrani kwa Sima70 ambaye ametoa majibu mazuri na kwa mpangilio mzuri.

NB: Kuna kipindi Mwina Kaduguda akiwa Katibu Mkuu wa FAT aliamua kupeleka majina ya Simba na Mtibwa kushiriki michuano ya CAF baada ya kuona ligi ya Muungano (wakati huo ndio inatoa wawakilishi) itachelewa deadline, na CAF wakayapokea

Sasa hayo majibu mazuri ndio yanaondola hilo hitimisho la mtoa mada? Mimi bado naona kituko tu kwanini kusiwe na utarabu unaoeleweka kwamba ligi za chi wanachama wa CAF zisiishe kwa utaratibu ambao mambo kama haya hayajitokezi? Ulaya yapo mambo haya??
 
Hii ni soka la Afrika bwashee
Sasa hayo majibu mazuri ndio yanaondola hilo hitimisho la mtoa mada? Mimi bado naona kituko tu kwanini kusiwe na utarabu unaoeleweka kwamba ligi za chi wanachama wa CAF zisiishe kwa utaratibu ambao mambo kama haya hayajitokezi? Ulaya yapo mambo haya??
 
Hii ngoma ingetokea Tanzania halafu utopolo ndo kafanyiwa hvyo naona mashabiki wake viazi wanaoenda airport kupokea wageni wangekuwa washachoma moto nyumba ya karia.
 
Sasa hayo majibu mazuri ndio yanaondola hilo hitimisho la mtoa mada? Mimi bado naona kituko tu kwanini kusiwe na utarabu unaoeleweka kwamba ligi za chi wanachama wa CAF zisiishe kwa utaratibu ambao mambo kama haya hayajitokezi? Ulaya yapo mambo haya??
Mleta mada aliuliza kigezo gani kilitumika al ahly kucheza CL ndio maana nikamjibu kwa ufasaha kabisa

Pia mleta mada hakupaswa kuconclude kwa sababu yeye aliuliza kigezo kilichotumika, kikawaida huwezi kuconclude kitu ambacho hukijui, aliuliza kwa sababu hajui, sasa aliconclude kwa fact ipi wakati hajui?

Kwahiyo, wewe unachoongelea sio hoja ya mleta mada
 
Back
Top Bottom