Kwa muda mrefu kumekua na makelele mengi ya kuienzi lugha yetu adhimu ya Kiswahili hapa Afrika Mashariki. Bila shaka Tanzania inaongoza katika hizo harakati.
Pamoja na makelele hayo, jitihada zinazofanyika ni ndogo kulinganisha na kile kinachopaswa kufanyika. Tuanzie Tanzania. Lugha yetu ya taifa ni Kiswahili.
Jambo la ajabu mtu akishuka kuanzia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa J.K Nyerere atapokelewa na mabango mengi yalioandikwa kwa lugha ya Kiiengereza. Kutoka uwanja wa ndege hadi katikati ya jiji la Dar es Salaam mabango karibu asilimia 80 ni ya Kiingereza.
Ukija huku Uswahilini hadi kwa mama ntilie pameandikwa Kiingereza mfano mama chausiku cafe. Ukienda dukani kwa Mangi pameandikwa Mfano Massawe shop. Pembeni kuna saluni imeandikwa madenge Barbershop au Manchester haircutting salon.
Ukienda buchani pameandikwa mfano Mwita butcheray kwa mbele kuna mashine imeandikwa Kabwe posho milling. Vituko zaidi viko stendi za mabasi.
Unaweza pewa mtihani tafuta basi au ofisi ya tiketi iliyoandikwa kwa kiswahili upewe hata milioni moja amini usiamini unaweza usipate na hela ukaiokosa hivihivi. Kampuni za mabasi zote maarufu unazozijua Tanzania na Afrika Mashariki zimeandikwa kwa Kiingereza.
Kuanzia Dar lux, zuberi, Abood, Kisesa, Bunda Bus, Ally's, Nchambis, Happy Nation, Akamba, Mohammed, Scandnavia, Tanganyika na zinginezo unazozijua zote ni kwa Kiingereza.
Nyaraka nyingi za serikali na watu binafsi zimeandikwa kwa Kiingereza. Majina ya Taasisi za umma au watu binafsi asilimia kubwa ni Kiingereza. Nenda hadi vijijini huko unakuta Kaduka ka nyasi kameandikwa Chacha shop.
Wanaojenga barabara alama nyingi wameandika Kiingereza. Ukiwaambia madereva watafasiri ina maana gani hawajui zaidi ya mazoea tu kwamba hapa barabara inatengenezwa.
Angalia kwa makini risiti ya benki kuu aliyoandikiwa yule mchimbaji wa Tanzanite ndugu Saniniu Laiza yote imeandikwa kwa kiingereza wakati anayelipwa ni Mswahili. Watanzania wengi hawawezi kutafasiri hiyo lugha lakini jambo la ajabu ndiyo imezagaa kila kona ya nchi hii.
Kesi inaendeshwa kwa Kiswahili wakati hukumu inaandikwa kwa kiingereza!VMgeni yeyote kutoka ulaya, Asia au Amerika akifika Tanzania kwa muonekano wa maandishi kwenye mabango umwambie abahatishie ni lugha gani ya taifa ya nchi yetu bila shaka atasema ni Kiingereza! Timu zetu za mpira zote za ligi kuu ni mwendo wa Kiingereza tu.
Mara Simba sports club kule kwa watani Young Africans sports club yaani hadi timu ndogo kama Namungo na biashara zote zina maandishi ya Kiingereza. Matokeo yake Kiswahili kimedumaa ukuaji wake ni wa polepole.
Kama tungekua makini na kiswahili lugha hii ilitakiwa iwe inaongelewa sana hasa kusini mwa jangwa la sahara ambako tayari kulikua na mtaji wa Kiswahili.
Nchi kama Malawi, Zambia, Botswana na Msumbiji zilitakiwa ziongee sana Kiswahili badala yake Kiswahili kinaongewa sehemu chache katika nchi hizo hasa mipakani. Sehemu ijayo tutajadili vituko vilivyopo katika chi zingine za Afrika Mashariki zilizobakia.
Jamani, tuipende na kuithamini lugha yetu.