Afrika na utajiri wa Lugha

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,319

Ramani ya Lugha za Afrika, picha kwa hisani ya Nations Online

Afrika kuna utajiri mkubwa wa Lugha za kusemwa na binadamu, kati ya hizo kubwa kabisa ni Kiswahili, Lingala, Amharic, Yoruba, Zulu na Kiarabu (kama utakihesabu kuwa lugha ya Kiafrika).

Lugha kama Kiswahili tayari ina wasemaji zaidi ya milioni mia moja na imesambaa katika nchi zote za maziwa makuu. Nchini Tanzania tayari kuna mjadala mkubwa juu ya lugha ipi iwe ya kufundishia mashuleni na vyuoni na makundi fulani ya wanazuoni wanaonekana kupigia chapuo Kiswahili.

Lugha za Yoruba, Hausa na Igbo husemwa katika nchi moja lakini kigezo cha kuwa na wasemaji wengi tayari kinazibeba. Lingala inasemwa katika nchi mbili za Zaire na Angola ingawa lahaja au lugha zinazofanana nayo zipo pia katika nchi za Gabon na Kongo Brazaville.

Kwanini tumeendelea kutumia lugha za wazungu wakoloni wakati zipo lugha zetu, kubwa na ambazo zina msingi mzuri wa usanifishaji (kigezo cha urasmi). Lugha kama Kireno inazungumzwa na idadi ndogo tu ya watu huko Ulaya, katika nchi ilimozaliwa lakini hapa Afrika imepata wateja katika nchi tatu, Angola, Msumbiji na Cape Verde huku ikifurahia hadhi ya Lugha rasmi.

Lugha kama Kijerumani, inazungumzwa katika nchi chache tu Ulaya, lakini ni Lugha rasmi na inayotambulika, hali kadhalika mataifa mengi ya Ulaya wamekuwa wakitumia lugha zao hata kama hazina wazungumzaji wengi nje ya mipaka. Kwanini Afrika tufundishwe na tulazimishwe kuwasiliana kwa lugha ngeni hata kama zina ukakasi kwa wasemaji?

Tujadili kama kuna namna yoyote ya kuondokana na utumwa huu usio na sababu.

Hapa chini ni orodha ya nchi za Kiafrika na lugha zinazozungumzwa humo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…